Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zuchu alivyomdhibiti Diamond kitabia kwa miaka minne

STAA wa Bongofleva kutoka WCB Wasafi, Diamond Platnumz anatimiza miaka minne bila ya kutangaza uhusiano mpya tangu kuachana na Tanasha Donna kutoka nchini Kenya  2020.

Ni mara ya kwanza kwa Diamond kukaa kipindi kirefu bila kutangaza uhusiano mpya jambo liloibua tetesi za kuwa pamoja na warembo kama Mimi Mars, Zuchu, Andrea Abrahams wa Afrika Kusini na Fantana kutoka Ghana.

Tanasha ndiye mwanamke wa mwisho kwa Diamond kumtangaza yupo naye, Desemba 2018 ndipo wawili hao walipoutangazia umma kuwa wapo pamoja, na hadi wanaachana walikuwa amejaliwa mtoto mmoja, Naseeb Jr (2019).

Tetesi za Diamond kuachana na Tanasha zilianza Februari 2020, zilikolea baada ya Diamond kususia uzinduzi wa EP ya Tanasha, DonnaTella EP (2020) uliofanyika Nairobi na kufikia Machi, Tanasha akaweka wazi hawapo pamoja.

Kabla ya kuwa na Tanasha, Diamond alikuwa na uhusiano na Zari ‘The Bosslady’ kutoka Uganda ambaye wamejaliwa watoto wawili, Tiffah na Nillan. Na huu ndio uhusiano uliodumu kwa miaka mingi tangu 2014 hadi 2018.

Tangu kuachana na Tanasha, Diamond amekuwa akihusishwa kuwa na uhusiano na Zuchu, ukaribu wao wa kikazi na hata jinsi wanavyoweka mambo yao mitandaoni vinatoa picha huwenda jambo hilo lina ukweli.

Hata hivyo, Mama mzazi wa Diamond, Bi Sandra ‘Mama Dangote’ na mama yake Zuchu, Khadija Kopa kwa nyakati tofauti wamekanusha vikali wawili hao kuwa pamoja katika uhusiano na kusema ni mtu na bosi wake na ndicho pekee wanachofahamu.

Kwa mujibu wa Mama Dangote, Diamond hajawahi kumtambulisha Zuchu kwake kama mpenzi wake kitu ambacho alikifanya alipokuwa na Wema, Zari na Tanasha, hivyo anajua mwanaye anamsimamia Zuchu kimuziki chini ya WCB Wasafi na si vinginevyo.

Ila kama ni kweli wawili hao wapo pamoja, basi Zuchu atakuwa amembadili Diamond kitabia kwa kiasi kikubwa maana hakuna taarifa za usaliti kati yao zilizovuja kitu ambacho Zari, Wema Sepetu na Penny walilia vilivyo walipokuwa na Diamond.

Penny alilia kwa Diamond kumsaliti na Wema naye Wema akalia kwa Diamond kumsaliti na Jokate. Baadaye Zari akalia kwa Diamond kumsaliti na Hamisa Mobetto.

“Tuliachana baada ya kunisaliti na Jokate. Tulikuwa tunapendana sana. Kwake nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo nipo nayo hata kama sio mazuri. Nadhani pia inagharimu mwanaume akishajua anakutawala,” alikaririwa Wema akizungumzia kuhusu kuachana na Diamond.

Naye Zari alisema: “Nimeamua kusitisha uhusiano wangu na Diamond. Tumetengana kama wapenzi, lakini sio kama wazazi. Nitawafundisha wanangu wanne kuwaheshimu wanawake kila wakati na kumfundisha binti yangu maana ya kujiheshimu.”

Ila hadi sasa hakijasikika kilio cha Zuchu, inaonyesha kuwa yupo katika mikono salama na amefanikiwa kumdhibiti mtu wake. Nyimbo zake kama Sukari, Nyumba Ndogo, Mwambieni, Cheche, Jaro, Fire, Love, Utaniua na kadhalika zinathibisha hilo kwa kiasi chake.

“Mkubwa kwenu ninyi ila kwangu hana kauli,” ni moja ya mistari kutoka kwenye wimbo wa Zuchu, Fire (2022) unaopatikana katika mradi wake wa 4:4:2.Je, ni kweli Diamond ni mkubwa (Bosi) kwa wasanii wengine hasa wa WCB Wasafi ila hana kauli kwa Zuchu kisa penzi lao la siri? Kupitia muziki wao tunaweza kupata picha ya suala hilo kwa kiasi fulani.

Katika nyimbo zote 10 kutoka kwenye EP ya Diamond, First of All (FOA) (2022, hakuna wimbo hata mmoja Diamond analalamika kuumizwa na mapenzi, zote anajipambanua kama mtu anayefurahia zaidi mapenzi kwa sasa.

Kwenye EP hiyo uandishi wa Diamond umebadilika sana, ni tofauti na albamu zake tatu, ‘Kamwambie’, ‘Lala Salama’ na ‘A Boy From Tandale’. Huku nyimbo za kulia na mapenzi zipo za kutosha kama ‘Mbagala’, ‘Nalia na Mengi’, ‘Mawazo’, ‘Kizaizai’, ‘Kosa Langu’ n.k.

EP hii ameshirikishwa msanii mmoja tu wa kike ambaye ni Zuchu aliyeshirikiana naye kwenye wimbo ‘Mtasubiri’ ambapo wanasisitiza kwao hakuna kuachana, huku Zuchu akikiri anasikia maneno kuwa Diamond hajatulia (kicheche), ila wanaosema hayo, hayawahusu.

Na katika msimu uliopita wa tamasha la Wasafi Festival, Zuchu ndiye msanii pekee wa kike mkubwa wa Bongofleva aliyepata nafasi ya kutumbuiza katika shoo zote, aliposema, “kubwa kwenu ninyi ila kwangu hana kauli” hiki ndicho alichomaanisha?

Tangu amemsaini Zuchu katika lebo ya WCB Wasafi hapo Aprili 2020, Diamond hajafanya kolabo yoyote na msanii mwingine wa kike ni yeye na Zuchu tu ambaye wameshirikiana katika nyimbo tatu Cheche (2020), Litawachoma (2020) na Mtasubiri (2022).

Katika wimbo wa Utaniua (2023) ambao Diamond katokea katika video yake na kucheza uhusika wa mpenziwe, Zuchu anasema penzi lao lilianza tu kama utani wala hakudhani utafika wakati akiwa hapatikani anashindwa kula na hata kulala. Hii ni ishara tosha kuwa kila mmoja kampata mwenzake ila Mondi kapatikana zaidi.