Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wizkid ndiye Messi ila sio Diamond wala Harmonize

Muktasari:


  • Staa wa Argentina, Lionel Messi ni mfano hai katika hilo, ameshinda Kombe la Dunia 2022, Copa America 2021, Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) (4), Ligi Kuu Hispania (La Liga) (10), Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1) (2) na tuzo saba za Ballon d’Or.

Katika mchezo wa soka mchezaji akishinda kombe la dunia, kombe la bara lake kwa ngazi ya timu ya taifa na klabu, ligi ya ndani pamoja na tuzo ya Ballon d’Or, tunaweza kusema amepata mafanikio katika kazi yake kwa asilimia 99.


Staa wa Argentina, Lionel Messi ni mfano hai katika hilo, ameshinda Kombe la Dunia 2022, Copa America 2021, Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) (4), Ligi Kuu Hispania (La Liga) (10), Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1) (2) na tuzo saba za Ballon d’Or.


Ukija katika filamu, kushinda tuzo za Oscar ambazo zimekuwa zikitolewa tangu mwaka 1929 ni ndoto ya kila muigizaji, tuzo hizi zilizotengenezwa kwa dhahabu halisi yenye uzito wa karati 24 ndizo za juu zaidi upande wa filamu duniani.


Na katika muziki kila msanii anatamani kushinda tuzo ya Grammy na hata kuchaguliwa kuwania tu, kila mwanamuziki anatamani wimbo wake uwe namba moja chati kubwa kama za Billboard Hot 100 au albamu yake kuwa namba moja Billboard 200.
Kwa msingi huo, mshindi wa Grammy kutokea Nigeria, Wizkid ni mfano halisi wa Messi katika kazi yake na sio sawa na Diamond Platnumz na Harmonize ambao waliwahi kuingia katika mvutano kuhusu ni wimbo upi wa Amapiano Bongo ambao umefanya vizuri kimataifa.


Utakumbuka Wizkid ameteuliwa mara tatu kuwania tuzo za Grammy na kushinda mara moja kupitia wimbo, Brown Skin Girl (2019) aliyoshirikishwa na Beyonce Knowles kutoka katika albamu yake, The Lion King: The Gift.


Diamond anaamini wimbo wake, Shu! (2023) ndio uliofanikiwa zaidi kuliko wowote wa Amapiano. Harmonize anapinga kwa madai wake, Single Again (2023) ndio wenye mafanikio kutokana wote umeimbwa kwa lugha ya Kiingereza na bado ukapendwa.

 
Wizkid anasikia mvutano wao na kuamua kuwapa somo kupitia wimbo wake, Essence (2020) akimshirikisha Tems kutoka katika albamu yake ya nne, Made In Lagos.


Anasema bado ni mapema kwa Diamond na Harmonize kujigamba nyimbo zao zimefanikiwa kimataifa wakati hatuzioni katika chati kubwa za muziki duniani na wala hazijashinda tuzo zozote, sio tuzo kubwa tu kama Grammy bali hata za ndani kama TMA.


Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita hakuna wimbo kutokea barani Afrika uliofanya vizuri duniani kama ‘Essence’ wa Wizkid, Diamond na Harmonize wakitaka kujua nyimbo zao zimefanya vizuri kimataifa, basi ‘Essence’ iwe kipimo chao.


Wimbo huo umeshinda tuzo tuzo mbili za All Africa Music Awards (Afrima) 2021 kama Wimbo Bora wa Mwaka na Wimbo Bora wa Kushirikiana. Na umeshinda tuzo tatu za African Entertainment Awards USA (AEAUSA) 2021 kama Wimbo Bora wa Kushirikiana, Video Bora na Wimbo Bora wa Mwaka.


Umeshinda tuzo mbili za NAACP Image Awards 2022 kama Video Bora na Wimbo Bora wa Kimataifa, umeshinda The 3Music Awards 2022 kama Wimbo Bora Afrika, umeshinda BET kama Wimbo Bora wa Kushirikiana.


Vilevile umeshida tuzo mbili za American Music Awards 2022 kama Wimbo Bora wa R&B, huku Wizkid akishinda kama Msanii Bora wa Afrobeats na kuandika rekodi kama msanii wa kwanza Afrika kufikia mafaniko hayo.


Umefanya vizuri chati kubwa duniani, umeshika namba moja Billboard US Afrobeats Songs, namba tisa Billboard Hot 100, namba 11 US Rolling Stone Top 100, namba 28 Billboard Global 200 na namba moja Billboard US World Digital Song Sales n.k.


Na kwa matokeo hayo ‘Essence’ umeandika rekodi kama wimbo wa kwanza nchini Nigeria kuingia chati za Billboard Hot 100 na Billboard Global 200 kwa wakati mmoja, huku ukiwania tuzo ya Grammy 2022 kama Wimbo Bora Duniani.


Kwa kifupi ‘Essence’ ndio wimbo pekee uliompatia mafaniko zaidi Wizkid katika taaluma yake ya muziki tangu kutoka kwake, ndio wimbo uliomfikisha katika kilele cha mafanikio ya kazi yake. Je, ‘Shu!’ na ‘Single Again’ za Diamond na Harmonize zimefanya hivyo?.


Utakumbuka Wizkid ameshinda na kutunukiwa tuzo zaidi ya 145, ameuza rekodi zaidi ya milioni 50, ana rekodi nne za dunia za Guinness huku akishirikisha wasanii wakubwa duniani kama Beyonce, Drake, Justin Bieber, Chris Brown n.k.


Ikumbukwe Wizkid ameshinda na kutunukiwa tuzo zaidi ya 145, ameuza rekodi zaidi ya milioni 50, ana rekodi nne za dunia za Guinness, amejaza kumbi duniani kama 02 Arena, Madison Square Garden, Ziggo Dome, Accor Arena n.k, huku akishirikisha wasanii wakubwa duniani kama Beyonce, Drake, Justin Bieber, Chris Brown n.k.