Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aslay hataki kushobokea tena

ASLAY Pict

Muktasari:

  • Staa huyo wa Mhudumu, Natamba na Usinitie Doa, amesema tabia ya kushobokea mademu wa nje ya nchi hana mpango nao tena, baada ya mazito kumkuta alipojiwekwa kwa Mnigeria na kujikuta akiishia njiani kabla mahaba hayajakolea.

WALIOSEMA aisifiaye mvua imemnyeshea, wala hakukosea baada ya nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini aliyeibuliwa na Kituo cha Mkubwa na Wanae kisha kutamba na Yamoto Band, Aslay kufichua jambo ambalo wengi hawakuwa wanalifahamu.

Staa huyo wa Mhudumu, Natamba na Usinitie Doa, amesema tabia ya kushobokea mademu wa nje ya nchi hana mpango nao tena, baada ya mazito kumkuta alipojiwekwa kwa Mnigeria na kujikuta akiishia njiani kabla mahaba hayajakolea.

Akipiga stori mbili tatu na Mwanaspoti, Aslay alifichua kuwa miaka saba iliyopita aliwahi kupata mpenzi wa kike kutoka Nigeria, aliyefikia hadi kuja hapa nchini, lakini sharti la kumtaka awe anamposti katika mitandao ya kijamii, lilimshinda na kujikuta wakitemana hata kabla mambo hayanoga zaidi.

Aslay alisema kitendo cha yeye (Aslay) kumchomolea sharti hilo ambalo kwake aliona ni adhabu kubwa, ilimfanya bibie kususa na penzi lao kuvunjika mapema.

“Mapenzi na wanawake wa nje ya nchi sitaki, niliwahi kumpata mchumba wa Nigeria, lakini tuliachana kisa nimekataa kumposti katika mitandao ya kijamii maana naona alitaka umaarufu kupitia kwangu, baada ya kukataa, penzi likaishia hapo na sina mpango nao tena hata akitokea mwingine,” alisema.

Aidha, mwimbaji huyo anayetamba kwa sasa na ngoma ‘No Money No Love’ aliwataka wasanii wenzake kuwa makini kwani wanawake wa nje hasa wanaopatikana mitandaoni baadhi yao sio wazuri na huwa na lengo la kuwatumia kwa manufaa binafsi na mwishowe wanaenda kuolewa na wanaume wa kwao.

Hata hivyo, wakati Aslay akitoa ushauri huo, tayari kuna mastaa kibao wanafurahia maisha na wapenzi raia wa kigeni kama Jux liyefunga ndoa na Mningeria Priscilla Ajoke Ojo, ilihali zilipendwa wake, Vanessa Mdee anaendelea kula maisha na Mmarekani mwenye asili ya Nigeria, Rotimi.