Whozu aachia wimbo wa Simba Day

MSANII wa muziku wa Bongofleva, Whozu ameachia wimbo maalum ‘Simba ni noma’ maalum kwa ajili ya siku ya Simba inayotarajia kufanyika Septemba 19 mwaka huu.

Wimbo huo Whozu ameshirikiana na msanii Mwanza Donat raia wa Congo anayetamba na wimbo wa Bana Congo wenye staili ya bolingo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kutangazwa tarehe rasmi ya kutambulishwa kwa jezi, Whozu amesema wimbo huo ameamua kuufanya kutokana na mafanikio ya klabu hiyo.

“Kutokana na mafanikio ya Simba na mimi nimeona nitengeneze wimbo kwa  ajili ya wachezaji kujivunia mafanikio lakini pia na Simba yenyewe kiujumla maana mimi pia ni shabiki wa klabu hii,” amesema Whozu

Whozu amesema kwenye wimbo huo ambao ameshirikiana na msanii wa Congo, Donat amesema ameangazia staili tofuti kwa ajili ya mashabiki wa klabu hiyo.

“Nimetumia ubunifu kwenye wimbo huu, wenzetu wanatumia singeli, mimi nimechanganya Singeli, Bongo fleva na bolingo na hii kutokana na Simba kuwa na mashabiki aina tofauti tofauti,” amesema Whozu.

Whozu amesema kufanya kazi na Donat haikuwa tabu kwa sababu msanii huyo na yeye ni shabiki wa Simba.

“Uongozi wangu ulipoongea na yeye haikuwa tabu sana, nilimuambia tuurudie wimbo wa Bana Congo na akakubali, ameimba kiswahili kwenye wimbo wetu,” amesema Whozu.