Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WENGE MUSICA BCBG; Mbuyu usiofutika licha ya kuvunjika - 3

KATIKA mfululizo wa makala ya simulizi ya kundi la Wenge Musica BCBG, lililoteka na kuwapagawisha mashabiki na wapenzi wa muziki wa lingala kutokana na ngoma zao kali, tuliona jinsi walivyofanya tamasha lao la kwanza na jinsi mambo yalivyoanza kuchanganya.
Pia tuliona namba kundi hilo lilivyokuwa kama Victoria Eleison moja ya makundi yaliyobamba sana enzi hizo na jinsi Wenge Musica BCBG lilivyojipatia umaarufu mkubwa.
Tunaendelea kuona jinsi mambo yalivyo kundi na safari yao iliyokuja kutamatika rasmi mwaka 1997 na kuwaacha mashabiki wakiwa na kiu kubwa dhidi yao kwa umahiri waliouonyesha kupitia kazi zao mbalimbali. Tiririka nayo...!
 

Na katika kipindi hiki, Patient Kusangila alijiunga na kundi kama mpiga gitaa la rhythm sababu ikiwa kundi lilikuwa tayari lina wapiga gitaa la besi watatu (ambao ni Didier Masela, Delo Bass na Christian Mwepu Mabanga)
Pia, Rapa wa kwanza wa kundi, Roberto Wunda alijiunga na Wenge kipindi hiki, akiwa na wenzake Full King na Kennedy wakitokea Kundil la Folkloric Group Bana Odeon.
Mpiga drums aliyekuja kujizolea sifa kibao, Titina El Capone ambaye alisoma na JB Mpiana na Blaise Bula alijiunga naye alijiunga na kundi hili. Rapa Kennedy hakumaliza muda akajitoa katika kundi na kwenda katika Kundi la Folkloric Group Swede Swede de Kentambo.


WALALA SELO
Muda mfupi kabla ya kurekodi albamu mwaka 1990, kundi hilo likapanga safari ya kwenda Ubelgiji kupitia Paris, Ufaransa kwa mara ya kwanza lakini wanamuziki wa kundi hilo walikamatwa jijini Kinshasa kwa sababu walikuwa na visa za uongo, visa feki na kuwekwa kizuizini kwa siku nzima, viongozi waliokamatwa ni JB Mpiana, Werrason, Makaba na Masela lakini waliachiwa baadaya Watoto wa Rais wa Congo wa wakati huo, Mobutu Sese Seko kuingilia kati. Watoto hao ambao ni Manda Mobutu ‘Maitre Madova’, Nzanga Mobutu ‘November’ na Jose Kongolo Mobutu ‘Saddam Hussein’ walikuwa ni marafiki wakubwa wa bendi hasa JB Mpiana na Werrason.
Kukamatwa kwao kulifanya waweke maneno haya katika wimbo wa Kin e Bouge "Wele oyo toyoka na sango to vivre yango ba jaloux basepeli basali feti bameli masanga, ba famille na biso mawa na mitema bakolelaka biso welewelewele."
Tafsiri: Kabla tulikuwa tumeona taswira ya magereza kwenye runinga, lakini sasa tumejionea halisi, maadui zetu wanasherehekea kwa kunywa bia wakati familia zetu zikitulilia.”


YAENDA ULAYA
Katika safari hii waliofanikiwa kuingia Ulaya na hati feki ni wawili tu ambao ni mpiga dramu, Pipo la Musica na mwimbaji, Ricoco Bulambemba.
Huko Ufaransa, Ricoco Bulabemba na Pipo la Musica, wakaungana na Alain Mwanga ‘Zing Zong’ na Aime Mbwanga waliokuwa wamemaliza masomo na kuanza mazoezi ya pamoja.
Na ni kipindi hiki Alain Mwanga na Aime Mbwanga waliwasajiri waimbaji kama Ya yuyu, JDT Mulopwe, Savanet Depitsho na Rento Vena, mpiga kinanda Nzenze, mpiga gitaa la besi, Boss Matuta na mpiga gitaa la rhythm Lidjona, Adolphe Dominguez naye alikuwa ni miongoni mwa walioshiriki mazoezi haya huko Paris.


ISHU YA USHIRIKINA
Julai 1990 Kinshasa, sitafahamu ikaibuka katika kundi baada ya mpiga gitaa la pili, Blaise Kombo kufariki kwa ajali ya gari wakati akirejea nyumbani kutoka kwenye moja ya shoo za Wenge Musica.
Hii ilileta mkanganyiko sana sababu baadhi ya wanachama wa kundi hili walikuja kunukuliwa kuwa ajali hii ilipangwa na ilikuwa ni nani atakayekuwa wa kwanza kupanda stejini siku hiyo ya shoo ndiye atakayefariki na Blaise Kombo alikuwa wa kwanza kupanda stejini kwenda kutesti sauti ya gitaa lake akifuatiwa na Maradona.
Baada ya tukio hili Maradona na Delo Base walijitoa katika bendi.


YATUA PARIS
Mwaka 1991 hatimaye bendi ikafanikiwa kufika Paris bila uwepo wa Manda Chante, rapa Full King na Alain Mpela (aliyekuwa kwenye mitihani na nafasi yake ikachukuliwa Marie Paul Kumbulu), Wakarekodi albamu ya Kin e Bouger iliyokuwa na mafanikio makubwa, huku JB Mpiana akipata tuzo ya mwimbaji bora kutoka Congo.
Moja ya kivutio katika albamu hii ya Kin e bouge ni kuwepo kwa waimbaji watatu waliokuwa na sauti nzito (Werrason, Marie Paul na Blaise Bula) ambao wanaimba pamoja na kung’ara.
Baada ya albamu hii Adolphe Dominguez akajiunga na bendi kwa mara nyingine baada ya masomo huku Marie Paul Kumbulu akijitoa jumla katika bendi akihisi kutothaminiwa na viongozi wa bendi.
Marie Paul Kumbulu akaungana na Alain Mwanga, Aime Mbwanga na Bulambemba, muda mfupi rapa Full King aliyekuwa amejitoa Wenge Musica muda mrefu, akajiunga.
Ujio wa Marie Paul ukabadilisha mtazamo kutoka mazoezi na kuunda kundi la Wenge Musica Aile Paris, baadaye walikuja kurekodi albamu ya kwanza ya Wenge Musica Aile Paris iitwayo Molangi ya Malasi (Chupa ya Manukato), wimbo ambao uliotungwa na Ricoco Bulambemba na ulitakiwa kuwemo katika albamu ya Kin e Bouge ya Wenge.


MGOGORO WAIBUKA
Mwaka 1992 wakatoa albamu ya pili iitwayo Nganga Nzambe na baadaye Maradona aliyekuwa amejitoa Wenge siku nyingi, akajiunga Wenge Aile Paris.
Mwaka 1993 mgogoro ukaibuka na kumfanya Aime Bwanga ajitoe na kuunda kundi lake liitwalo Wenge Musica Aile Paris Kumbela, na ni kipindi hiki Manda Chante naye akajitoa Wenge Musica 4x4 BCBG baada ya albamu ya Kalayi Boieng kutoka.
Huko Ufaransa Manda Chante akajiunga na Ricoco, Alain Mwanga na Marie Paul na kubadili jina kutoka Wenge Aile Paris (Paris-based wenge) kutokana na kujitoa kwa Aime Mbwanga na kuwa Wenge El Paris (Wenge Mfalme wa Paris).
Tukirudi upande wa Wenge Musica BCBG baada ya Kin e Bouge kutoka, Mwaka 1992 kundi likarekodi albamu ya Pleins Feux huko Ubelgiji ikiwa na nyimbo kama Djolino ya Werrason, Dady Bitodi (Djolina), Ave Maria  (Blaise Bula) na nyingine nyingi.
Ni katika albam hii mpiga gitaa la pili, Fifi Mwamba ‘Ficarré Ngenge’  na mpiga kinanda Desire Kalala walijiunga na kundi na kushiriki katika kurekodi, pia mwimbaji Manda Chante alishiriki katika albamu hii.
Albamu hii ilirekodiwa tu na haikutoka kwa wakati sababu ikiwa ni mgogoro kati ya moja ya watoto wa Mobutu ambaye ni Jose Kongolo Mobutu ‘Saddam Hussein’.


MGOGORO NA MTOTO WA RAIS
Chanzo cha mgogoro huu inaelezwa ni mwanamke aliyekubali kuwa mpenzi wa JB (kabla JB hajawa na uhusiano na Amida Shatur).
Mwanamke huyo alidaiwa kumkataa mtoto wa Rais, Kongolo Mobutu, hivyo naye akaamua kuwaadhibu kwa kutoruhusu albamu hii kwenda sokoni mpaka pale mwanamke huyu alipokubali kuwa upande wake.


MANDA CHANTE NA MADAI MAZITO
Albamu hii ilikuja kuingia sokoni miaka minne tangu irekodiwe, baada ya kutoka Kalayi Boing (1993) na Les Anges Adorables (1994) kuwa zimetoka mwaka 1993 kundi likarekodi albamu ya Kalayi Boeing huko Ulaya na kutoka mwaka huohuo, muda mfupi baada ya albamu hii kutoka, Manda Chante (anayesika sana katika Wimbo wa Kalayi Boieng) akajitoa na kujiunga Wenge El Paris (Rejea maelezo ya hapo juu).
Alijitoa baada ya viongozi wa kundi kutoonyesha ushirikiano wowote alipougua ugonjwa wa ajabu wa ngozi (Tete kuwanga).
Manda Chante alimshutumu sana Werrason kwa kushindwa kumlipa hela kipindi alichokuwa anaumwa. Pia, aliuhusisha ugonjwa huo na nguvu za giza, huku shutuma kali akizipeleka kwa JB Mpiana kuwa alitaka kumuua kutokana na sauti yake kupendwa sana wakati albamu hii inatoka.


EMELIA NA TUTU CALUDJI
Baada ya kujitoa kwa Manda Chante, kundi likarejea nyumbani na kuanza kutafuta mbadala wake.
Wengi wakajitokeza kwenye majaribio ili apatikane wa kuziba pengo lake. Baaadhi watu maarufu waliojitokeza katika usaili huo ni Babia Chokoro (ni mwanamuziki mwenza wa zamani wa Manda Chante huko Yoka Choc), Papy Sesele ‘Adjani sesele’, Blaise Yombo Lumbu ‘Tutu Caludji’ na Aimelia Lias Miankodila ambaye alishinda kinyang’anyiro hicho na hivyo kuwa mbadala wa Manda Chante.
Lakini Tutu Caludji akapelekwa katika sekta ya rapa baada ya kuonekana pia anaweza kughani. Pia, baada ya albamu ya Kalayi Boieng, Alain Makaba aliamua kubaki Ulaya na kufanya makazi yake huko, hivyo Ficarré Mwamba akawa mpiga gitaa la solo kiongozi na baadaye Vincent Kasongo Mbokaliya ‘Burkina Faso’ akajiunga katika kundi.
Ni kipindi hiki Ali Mbonda alijiunga ili kuziba pengo la Don Pierrot aliyekua amejitoa wakati bendi ilipofanya ziara ya Ulaya mwaka 1992.
Mwaka 1994 kundi likarejea Ulaya tena kwa ajili ya ziara bila uwepo wa Tutu Caludji na Mboka Liya na kurekodi albamu iliyofuatia ya Les Anges Adorables ambayo ni moja kati ya albam bora kabisa za Wenge Musica (albamu hii ina kopi mbili).