Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasemavyo wasanii ziara ya Korea kusini

Muktasari:

  • Wasanii hao waliondoka nchini Julai Mosi na huko walikwenda kujifunza namna ya kufanya kazi zao na kujiimarisha kisanaa na uchumi.

SIKU chache baada ya kurejea nchini wakitokea Korea Kusini, wasanii wa filamu na Tamthilia kwa nyakati tofauti wamezungumzia ziara hiyo, wakimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuigharamia safari hiyo na mambo mengine.

Wasanii hao waliondoka nchini Julai Mosi na huko walikwenda kujifunza namna ya kufanya kazi zao na kujiimarisha kisanaa na uchumi.

Baadhi ya wasanii waliokwenda Korea Kusini ni Steve Nyerere kama Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Idris Sultan, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Monalisa, Irene Paul, Gertrude Mwita na Godliver Gordian na haya ni maoni yao kwa kile walichokwenda kufanya huko.


WEMA SEPETU

Amesema kuna haja ya wasanii kurudi shuleni, ili kuongeza ujuzi na maarifa yatakayowasaidia kuboresha kazi zao za filamu.

Pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufikiria kufanya mabadiliko makubwa katika sekta hiyo na kuwapa nafasi wasanii kwenda kwenye mafunzo na kuahidi hawatamuangusha.

“Watu wasifanye kazi kwa uzoefu tunahitajika kurudi shule namaanisha wasanii, wahariri, waandishi wa hadithi, waongozaji, naamini kuna kozi mbalimbali zinaweza kuwasaidia.”


MONALISA

Kwa upande wake alisema; “Tunahitaji kupata eneo kubwa lisilopungua ekari 200 kwa ajili ya kufanya shughuli zetu za sanaa, ambalo kutakuwa na kila kitu kwa maana ya vifaa vyote muhimu vitakavyohitajika kuandaa kazi zetu za filamu, pia tumejifunza namna ya kujitambua na kujipa thamani kama wasanii, yaani sasa hivi mtu akinihitaji kwa upande wangu lazima anitajie maeneo yenye hadhi za juu kwa ajili ya kukutana.”


STEVE NYERERE

“Nikizungumzia kwa upande wa maboresho ya sekta yetu ya filamu, tunaiomba  Serikali kuweka mikakati zaidi kugharimia utendaji kazi wa sanaa wa Tanzania kama walivyofanya Korea Kusini kwa kuweka bajeti ya uandaaji wa filamu zao hali iliyoibua na kuendeleza sekta hiyo na ili kuwa wakubwa na kutangaza kampuni na viwanda vyetu, watumike wasanii wa ndani kutangaza shughuli zao.”


IDRIS SULTAN

“Ziara hii ililenga zaidi kujifunza na kubadilishana ujuzi na wasanii wa nchi hiyo, kwa kuzingatia filamu za Korea zina nafasi kubwa sana katika soko la filamu duniani.”


IRENE UWOYA

“Kwanza tuna mpongeza Rais Samia kwa kutupa fursa kwenda kujifunza zaidi kuhusu sanaa na tunaamini tulichojifunza huko kitatusaidia katika shughuli zetu za sanaa.”

Safari hiyo imekuja baada ya Rais Samia kutangaza neema kubwa kwa wasanii ya kugharamia safari zao pindi atakapokuwa na ziara za kikazi nje ya nchi.