Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waluguru Original Band waja na Plan B

Muktasari:

  • BENDI ya muziki wa dansi ya Waluguru Original yenye maskani mjini Morogoro, imefyatua ngoma mpya iitwayo Plan B inayotarajiwa kuachiwa rasmi hewani wikiendi hii.

BENDI ya muziki wa dansi ya Waluguru Original yenye maskani mjini Morogoro, imefyatua ngoma mpya iitwayo Plan B inayotarajiwa kuachiwa rasmi hewani wikiendi hii.

Rais wa bendi hiyo, Deogratius David 'Killer Boy' ameliambia Mwanaspoti kuwa, wimbo huo utaachiwa rasmi Jumamosi wakati Waluguru ikiingia chimbo kurekodi video yake itakayoachiwa wiki mbili zijazo.

Killer Boy amesema wimbo huo mpya umerekodiwa katika studio za AI zilizopo chini ya Prodyuza, Erasto Mashine mapema mwezi huu kabla ya aliyekuwa mpiga solo wao, Kinde Makengele kuondoka kwenda kujiunga na Bogoss Musica ya Nyoshi El Saadat.

"Kuna kazi kadhaa tumeziandaa, lakini tutakayoiachia wikiendi hii ni 'Plan B' ambayo video yake itakuwa imekamilika wiki mbili zijazo, kwani Waluguru kwa sasa ni mwendo wa bandika bandua," amesema Killer Boy, mwimbaji na nyota wa zamani wa bendi ya Levent Musica 'Wazee wa Kumuvuzisha' iliyokuwa na maskani katika hoteli ya Savoy. Kwa sasa Levent haipo katika ulimwengu wa muziki.

Alipoulizwa juu ya pengo la mpiga solo, Kinde Makengele aliyejiunga na Bogoss siku chache zilizopita na aliyeshiriki kucharaza gitaa katika wimbo huo wa Plan B, Killer Boy amesema limeshazibwa.

"Kila kitu kipo sawa kwa sasa, kwani aliyekuwa akisaidiana na Kinde (Makengele) kupiga gitaa hilo la solo kundini, HD Solo ndiye aliyeziba nafasi hiyo, na hakuna pengo, kwani jamaa hajambo kwenye kucharaza gitaa hilo," amesema Killer Boy aliyeweka bayana bendi hiyo ya Waluguru kama kawaida kesho Ijumaa itawasha moto kwenye Ukumbi wa F2 Florida, uliopo Msamvu, Morogoro na Jumamosi hii watakuwa New Terminal Pub, pia Msamvu kabla ya Jumapili watamalizia kazi F2 Florida.