Vanita Omary sasa yuko kamili

MWIGIZAJI na mpambaji wa wasani wa filamu za Swahiliwood, Vanita Omary, ameamua kuingia rasmi katika uandaaji wa filamu kama wafanyavyo wengine. “Mfumo wa filamu Tanzania haupo sawa, inakulazimu kufanya kazi nyingi kwa pamoja ili angalau kupata fedha kidogo za kuendesha maisha," alisema. "Kwa hiyo mimi na mume wangu Mr. Paul Mtindah tumeamua kufanya kazi zetu kwa maslahi ya familia, tumeanza na filamu ya 5 Questions niliyocheza mwenyewe na kuwashirikisha wasanii wengine." Kwa sasa msanii huyo amesema kuwa atajikita zaidi katika fani yake ya upambaji ambayo ndiyo taaluma yake aliyosomea. Pia alisema atawafundisha wapambaji wengine ili kuikuza fani hiyo yenye watalamu wachache. Vanita anatunga hadithi za filamu na mumewe ni mwongozaji wa filamu.