Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TUONGEE KISHKAJI: Kwanini Watanzania wanalalamika kuhusu Bongo Movie Korea?

Muktasari:

  • Wakati wakiwa huko wakijifunza, huku Tanzania wananchi tulikuwa tunalalamika kuhusu kodi zetu zinavyotumiwa na wasanii hao. Ilikuwa kila ukiingia katika mitandao ya kijamii Instagram na Twitter watu wanalalamika ni kwa kiasi gani safari hiyo haikuwa na tija kwa taifa na kuwa imetumia kodi zetu.

HIVI karibuni wasanii wa Bongo Movie walikwenda Korea Kusini katika ziara ya mafunzo iliyoratibiwa na Bodi ya Filamu Tanzania. Ziara hiyo ilikuwa na awamu mbili. Ile ya kwanza walikwenda wasanii kama Leah Richard ‘Lamata’ na Elizabeth Michael ‘Lulu’. Na safari ya pili walikwenda wasanii kama vile Irene Paul, Steve Nyerere, Eliud na wengine.

Wakati wakiwa huko wakijifunza, huku Tanzania wananchi tulikuwa tunalalamika kuhusu kodi zetu zinavyotumiwa na wasanii hao. Ilikuwa kila ukiingia katika mitandao ya kijamii Instagram na Twitter watu wanalalamika ni kwa kiasi gani safari hiyo haikuwa na tija kwa taifa na kuwa imetumia kodi zetu.

Kusema ukweli, baadhi ya watu walikuwa wakionekana wenye hasira sana na safari hiyo. Na sio watu wa kawaida tu, hata wasanii ambao hawakuchaguliwa kwenda katika safari walikuwa wanalalamika na kuonyeshwa kuchukizwa karibu na kila kitu kuhusu safari hiyo.

Kwa wasanii, wengi wanalalamika kwamba wenzao waliopelekwa Korea Kusini hawakustahili. Wanadai mtu kama Steve Nyerere kwa sasa hafai hata kuitwa mwigizaji au mtengeneza filamu kwa sababu hawakumbuki hata mara ya mwisho Steve alishiriki kwenye filamu ilikuwa lini.

Binafsi nilishangazwa na malalamiko hayo kwa sababu sikuona ubaya hata mmoja wa safari hiyo.

Safari imeratibiwa au imeandaliwa na Bodi ya Filamu. Bodi ambayo moja ya majukumu yake ni kuwatengenezea mazingira mazuri ya kazi na uandaaji watengeneza filamu wa Tanzania. Na moja ya namna ya kufanya hivyo ni kuwapatia elimu na mafunzo kuhusiana na tasnia hiyo.

Swali langu sasa kwanini wasanii kwenda Korea ionekane kama vile kodi zinatumika vibaya?

Nauliza swali hilo kichokozi tu, lakini sina haja ya kupewa jawabu kwa sababu nadhani najua kwanini. Kuna sababu mbili.

Kwanza, kwa wasanii wanaolalamika nadhani malalamiko yao hayana mashiko kwa sababu Tanzania kuna waigizaji zaidi ya maelfu na safari ilikuwa inahitaji idadi fulani chache ya wasanii.

Kwa hiyo hata angechaguliwa nani bado kuna wasanii wangekuwa hawajachaguliwa kwenda na walioachwa wangekuja na sababu za kwanini waliochaguliwa hawakustahili kwenda nchini humo.

Na kwa watu ambao sio waigizaji, nadhani malalamiko yao yanakuja kwa sababu safari hiyo iliwekwa kisiasa sana kiasi kwamba watu walidhani  pesa zao zinatumika - pesa ambazo zilitakiwa ziwajengee barabara, zinunue dawa.

Lakini uhalisia ni kwamba, safari za namna hiyo sio kama msiba, haziji ghafla.

Hizo ni safari ambazo zipo kwenye ratiba ya bodi na mara nyingi hutumia bajeti ya bodi ambayo hata kama inatoka kwa serikali ambayo ni kodi zetu, bado inafanya kazi ya kitaifa. Kazi ya kukuza utamaduni wa nchi yetu.

Filamu kama ilivyo sanaa zingine zimekuwa ni eneo kuu linalokuza utamaduni na kulitangaza taifa. Kwa hiyo swali ni je kuna ubaya gani wa kutumia kodi zetu kulitangaza taifa ili baadaye zirudi kwa njia ya utalii na kadhalika.

Nadhani cha kufanyia kazi ni kwanza wasanii kupunguza ubinafsi. Kama hujachaguliwa kwenye safari moja usitafute sababu za kwanini aliyechaguliwa hastahili.

Pili, tupunguze kuzifanya hizi safari kuwa ni za kisiasa badala yake ziwe safari za mafunzo kwa ajili ya kuwainua wasanii wetu na tasnia kwa ujumla.