Sonia wa Monalisa afanikiwa kutoka Ukraine

Wakati serikali ikieleza leo kuwa imefanikiwa kuwaondoa wanafunzi wote nchini Ukraine, Sonia ambaye ni mtoto wa msanii wa filamu, Yvonne Cherrie ’Monalisa’ ni mmoja wa waliofanikiwa kutoka nchini humo.
Hayo yamebainishwa leo na Jumatano, Machi 9, 2022 na Monalisa kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Monalisa ameandika ”Sasa naweza kula chakula kikashuka, naweza kujilaza nikapata usingizi maana binti yangu yupo salama nje ya mipaka ya nchi ya Ukraine. Alifanikiwa jana usiku kuingia nchi ya jirani yeye na wenzie wachache na wapo salama,"
“Napenda kuwashukuru wote waliokuwa nasi katika kipindi kigumu ambacho tumepitia, hakika kilikuwa kipindi kigumu hasa, kama haukuwa na ndugu yoyote Ukraine ulikuwa unaona kama kichekesho tu kinachoendelea kwakuwa pengine sisi Tanzania (ikiwemo mimi mwenyewe) hatujawahi kujua hasa maana halisi ya neno vita na tuendelee kuombea sana Taifa letu katika hili,"