Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sir Nature ataja simamo wake kwa Mondi, akwepa skendo ya mtoto

Muktasari:

  • Albam ya ‘Nini Chanzo’ pamoja na vibwagizo vikali kwenye nyimbo za wasanii wengine wakubwa zilikuwa chanzo cha jina lake kupaa juu kwa juu karika anga la muziki wa Tanzania akiwa chini ya P-Funky Majani wa Bongo Records aliyeking'amua kipaji hicho na kukipaisha zaidi.

MIAKA 28  iliyopita, Juma Kassim 'Sir Juma Nature' a.k.a Kibla kutoka Temeke alikuwa moja kati ya wasanii watatu wenye majina makubwa zaidi katika muziki wa Bongo Fleva.

Albam ya ‘Nini Chanzo’ pamoja na vibwagizo vikali kwenye nyimbo za wasanii wengine wakubwa zilikuwa chanzo cha jina lake kupaa juu kwa juu karika anga la muziki wa Tanzania akiwa chini ya P-Funky Majani wa Bongo Records aliyeking'amua kipaji hicho na kukipaisha zaidi.

Nature, aliyekuwa Mfalme wa TMK wakati huo, aliitikisa Bongo baada ya kuanza uhusiano wa kimapenzi na Malkia wa tasnia ya maigizo wakati huo, ‘Sinta’.

Uhusiano huo ulikoleza umaarufu kutokana na masimulizi mengi yaliyokuwa yanaanikwa kwenye magazeti pendwa aka magazeti ya udaku.

Kila uchwao, ilikuwa ni habari ya Juma Nature na Sinta ndizo zinazouza zaidi magazeti hayo.

Kwa wale watoto wa 2000, huenda hii ikawa ni habari mpya kwao, lakini enzi hizo Sir Juma Nature na Sinta ndio iliyokuwa ‘couple’ maarufu iliyowahi kutikisa zaidi kama ilivyowahi kuwa kwa Wema Sepetu na Kanumba au Wema Sepetu na Diamond.

Hivi karibuni, Mwanaspoti lilipata nafasi ya kukutana na Nature na kufanya mahojiano maalumu ya mishe zake kwa sasa na stori nzima ya maisha yake ya kimuziki na nje ya fani hiyo na mwamba alifunguka.

Sir Nature alisimamia pale pale juu ya Diamond Platnumz na kuweka bayana tuhuma za kuwahi kumkataa mtoto na mwenyewe amesema hizo zilikuwa ni drama za kutaka kumharibia. Endelea naye...!


KAACHA MUZIKI

Mkongwe huyo wa Rap Cartoon (Rapu yenye vionjo vya vichekesho) amezungumzia ukimya wake na madai ya kuacha muziki kwa kusema;

"Hivi watu wakoje? Kwanza mimi sipo kimya, nafanya shoo sehemu mbalimbali, kuhusu kutoa nyimbo mpya, kosa siyo langu bali ya mashabiki ambao wanatutenga sisi wakongwe.

"Yaani unaweza kutoka wimbo mpya hapa, lakini watu wala hawashtuki na wimbo ni mkali.. we acha tu, mfano tu ukiachana nami, wee angalia wasanii wakongwe katika muziki huu, wangapi wametoka nyimbo na zimevuma kidogo tu au hazijavuma kama za wasanii wao sasa?" anahoji Nature na kufafanua;

"Hii ni kutokana na kushindwa kupata sapoti, yaani mashabiki wa sasa huwaambii kitu na wasanii wa sasa ila ndiyo hivyo kutesa kwa zamu na siyo kusema mimi nipo kimya.

"Kuhusu madai ya kuacha muziki nilishasema, siku natangaza kuacha muziki basi nitaingia katika siasa kwa kuwa nipo karibu sana na jamii na nitawashangaza watu kwenye hili na asikwambie mtu wasanii wanaotangaza kuacha muziki na kuendelea kuwepo wanatafuta huruma ya mashabiki, au wanawapima watapokeaje, unajua ni vigumu kwa mwanamuziki kuacha kufanya muziki, hivyo wasidanganye watu na kutafuta kiki kwa kujaribu kuacha muziki, mimi kiukweli madai hayo ya kuacha muziki siyo ya kweli kwangu,  bado nipo sana kwenye muziki."


SKENDO YA KUKATAA MTOTO

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii, kumeibuka skendo ya Nature kukataa mtoto ambaye mtoto huyo alijitambulisha hadharani baba yake ni mkongwe huyo wa Bongo Fleva. Hapa anafunguka.

"Habari gani hizo tena? Mimi sijawahi kukataa mtoto wala kutelekeza mtoto, kwanza hiyo habari mimi sijaisikia na siyo mambo yangu hayo ya hizo skendo, mimi tangu nimeanza kufanya kazi ya muziki, maisha yangu  ya muziki hayasukumwa na skendo za mitandao ya kijaami kama baadhi ya wasanii wengine.

"Maana wasanii wengi wanaopenda skendo hawajiamini na wao ndio chanzo cha kushusha thamani ya muziki nchini, ndiyo maana hadi sasa naepuka sana skendo zozote zile, sasa mambo ya mtoto yanakujaje tena kwa umri huu niliofikia?" anasema Nature.


KITU ASICHOKIPENDA

“Katika vitu nisivyovipenda kwenye maisha ya muziki ni kuishi kwa skendo, mambo kama haya huwa ni sababu ya kushusha thamani ya mtu na kazi yake.”

Mimi muziki ni maisha yangu na kazi inayonipa fedha za kujikimu na familia yangu, napenda kutoa kazi zenye viwango ndiyo maana mashabiki wananipenda na kuendelea kufuatilia kazi zangu,” anasema.

Azungumzia madai ya kuzidisha pombe na kushindwa kurekodi.

Habari iliyopo kwa sasa ni madai ya Nature kuzidisha unywaji wa pombe hadi kushindwa kutimiza majukumu yake ya kazi yake  muziki.

Madai hayo ambayo yanatoka kwa baadhi ya wanamuziki wenzake ni pale  wanapopanga kwenda kurekodi nyimbo ya pamoja, basi yeye mara nyingi hushindwa kutokea na wakati mwingine akitokea huwa amelewa na kushindwa kurekodi. Anaweza kupewa muda wa siku nyingine ili aje akiwa hajalewa, lakini hali inakuwa vilevile na biashara huishia hapo. Huyu hapa anazingumzia hilo.

"Huwa nashangaa sana kusikia hizo habari na hii ni moja ya kunichafua mimi ili nishindwe kufanya kazi na watu, wanasema Nature amekuja studio amelewa, mimi silewi ila huwa nakunywa na kujitambua vizuri kabisa.


NDOTO ZA KUSHINDANISHWA NA MONDI

Kuna kipindi cha nyuma, mkongwe huyu aliyewahi kutoa albamu tano ambazo ni Nini Chanzo (2001), Ugali (2003), Ubinadamu Kazi (2005), Zote Historia (2006) na Tugawane Umaskini (2009), aliwahi kusema hawezi kufanya ngoma ya pamoja Diamond hadi  watakaposhindana jukwaani ili kubaini nani mkali kati yao, analiambia Mwanaspoti ndoto yake na msimamo wake bado uko palepale kuhusu kushindanishwa.

"Sina mjadala zaidi ya kusema nalitaka bado pambano la kushindanishwa na Diamond Platnumz kwenye jukwaa moja ili tujue nani zaidi kwenye hii tasnia. Mimi sina vipengele muda wowote saa yoyote nipo tayari halafu mambo mengine ndio yafuate."


KITU CHAKE MSICHOKIJUA

"Mimi ni mtu wa aibu sana, mpole na msikivu, tofauti na baadhi ya watu wengi wanavyonichukulia, pia kabla sijaanza muziki, nilifanya shughuli mtaani kama kupasua mawe, kuuza chuma chakavu na kusukuma mikokoteni, hivyo nashauri tu wale wenye kuingia kwenye hii game wasikate tamaa, ipo siku watakuja kutoka tu maana mfano mimi kipindi hicho sikutegemea kama nitakuwa mwanamuziki mkubwa na kusepa na kijiji katika kila shoo."


AMBEBA FELLA

Kama hujui hili kutoka kwa Nature, ndiye aliyemuingiza Mkubwa Fella kwenye muziki na kuanza kusimamia wasanii kama meneja wao, Nature alimwomba Fella amsimamie kimuziki na ndipo kazi ya umeneja ikaanza.

Mkubwa Fella alipata wazo la kuanzisha kundi la TMK Wanaume baada ya wasanii wengi kutaka kumshirikisha Nature katika nyimbo zao maana sauti yake ilikuwa bidhaa inayouzika kirahisi wakati huo.