Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Charz Baba, Luiza Mbutu gumzo uzinduzi albamu ya Twanga

CHAZ Pict

Muktasari:

  • Kwa anayefuatilia harakati za bendi hiyo kwa karibu, si jambo la kushangaza kuwa wawili hao wamekuwa wakionekana mara kwa mara kwenye vikao vya maandalizi, mazoezi na mikakati ya kuhakikisha uzinduzi huo unakuwa wa aina yake. Lakini kwa mashabiki, hali hiyo imeibua maswali mengi huku kila mmoja akitoa tafsiri yake.

WIKI chache kabla ya uzinduzi wa albamu ya 16 ya bendi ya Twanga Pepeta, macho na masikio ya mashabiki wa muziki wa dansi yamehamia kwa kiongozi wa bendi hiyo, Charz Baba na Mkurugenzi wake, Luiza Mbutu, ambao wamekuwa gumzo kutokana na ukaribu wao katika maandalizi ya tamasha hilo kubwa litakalofanyika Agosti 7, 2026, Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Kwa anayefuatilia harakati za bendi hiyo kwa karibu, si jambo la kushangaza kuwa wawili hao wamekuwa wakionekana mara kwa mara kwenye vikao vya maandalizi, mazoezi na mikakati ya kuhakikisha uzinduzi huo unakuwa wa aina yake. Lakini kwa mashabiki, hali hiyo imeibua maswali mengi huku kila mmoja akitoa tafsiri yake.

CHA 05

VIKAO VYACHOCHEA MJADALA

Mbali na mazoezi ya kila siku, chanzo kimeliambia Mwanaspoti kuwa viongozi na baadhi ya wanamuziki wa Twanga Pepeta wamekuwa wakifanya vikao vya mara kwa mara kujadili kila hatua ya uzinduzi, kuanzia maandalizi ya jukwaa, orodha ya nyimbo hadi namna ya kuwafikia mashabiki.

Ni katika mazingira hayo ambapo Charz Baba na Luiza Mbutu wameonekana wakiratibu mambo mengi kwa pamoja, hali iliyowafanya baadhi ya mashabiki kuanza kuhoji ikiwa kuna siri yoyote nyuma ya pazia.

“Kila mtu ana tafsiri yake. Wapo wanaoona kuna jambo zaidi ya kazi, lakini ukweli ni kwamba maandalizi ya albamu hii yanahitaji watu kushirikiana kwa karibu kuliko kawaida,” anasema mdau mmoja wa muziki wa dansi.

CHA 04

MAZUNGUMZO HADI USIKU

Jambo lingine lililozua mjadala ni namna viongozi na wanamuziki wa bendi hiyo walivyoanza kutumia muda mwingi kuwasiliana na mashabiki, hata nyakati za usiku, kuwahamasisha kununua tiketi mapema.

Baadhi ya mashabiki walitafsiri hali hiyo kama ishara ya kampeni isiyo ya kawaida, huku wengine wakisema ni uthibitisho kuwa Twanga Pepeta imejipanga kuhakikisha ukumbi unajaa siku ya uzinduzi.

Walipoulizwa na Mwanaspoti kuhusu sababu ya kutumia muda mwingi kuzungumza na mashabiki, viongozi wa bendi walieleza kuwa ni mkakati wa kuwafikia wadau ambao mchana huwa wanakuwa bize na majukumu ya kazi.

“Tunatumia kila nafasi kuwasiliana na mashabiki wetu. Wapo ambao mchana wanakuwa kwenye shughuli zao na ni vigumu kuwapata. Ndiyo maana wakati mwingine tunazungumza nao hata usiku kuwapa taarifa za uzinduzi na tiketi. Tunataka kila shabiki apate nafasi ya kushiriki siku hiyo muhimu,” walieleza.

CHA 03

NYIMBO ZAANZA KUWASHA MOTO

Wakati gumzo hilo likiendelea, Twanga Pepeta tayari imewaachia mashabiki nyimbo nne zinazounda taswira ya albamu hiyo mpya. Nyimbo hizo ni Ca Va Bien ikiwa tayari ina video, Usinitoe Roho, Tone la Sumu na Dear Ex, ambazo tayari zimeanza kupokelewa vizuri na wapenzi wa muziki wa dansi.

Kwa mujibu wa viongozi wa bendi, nyimbo nyingine bado zinaendelea kupikwa studio kabla ya kukamilisha albamu hiyo ambayo imepewa matarajio makubwa kutokana na ubora wa kazi zilizokwisha kutoka.

CHA 02

MAZOEZI YA MWISHO YANAENDELEA

Kwa sasa wanamuziki wa Twanga Pepeta wamejikita kwenye mazoezi ya mwisho wakihakikisha kila kipengele kinakuwa tayari kabla ya Agosti 7.

Lengo ni kuwapa mashabiki onyesho litakalokwenda sambamba na hadhi ya albamu ya 16, huku waandaaji wakiahidi kutakuwa na ubunifu wa jukwaani, maonesho ya moja kwa moja na burudani itakayowaacha wengi wakisimulia kwa muda mrefu.

CHA 01

TIKETI ZAANZA KUUZWA

Tiketi za uzinduzi tayari zimeanza kuuzwa ambapo kawaida ni Sh30,000, VIP Sh50,000, VVIP Sh100,000, huku meza ya watu 10 ni Sh1,000,000.

Waandaaji wamewataka mashabiki kuwahi kununua tiketi ili kuepuka usumbufu wa dakika za mwisho, wakisisitiza kuwa uzinduzi huo ni sehemu ya historia ya Twanga Pepeta baada ya safari ndefu ya kuandaa albamu hiyo.


GUMZO LITAISHA AGOSTI 7?

Wakati baadhi ya mashabiki wakiendelea kutafuta tafsiri ya ukaribu wa Charz Baba na Luiza Mbutu, viongozi wa bendi wanasisitiza kuwa kinachopewa kipaumbele kwa sasa ni kuhakikisha uzinduzi unafanikiwa na mashabiki wanapata burudani yenye thamani ya fedha zao.

Hata hivyo, jambo moja halihitaji mjadala. Gumzo linaloizunguka Twanga Pepeta tayari limefanikisha jambo muhimu zaidi, limewafanya mashabiki wa muziki wa dansi kuhesabu siku kuelekea Agosti 7, watakapokusanyika Mlimani City kushuhudia uzinduzi wa albamu ya 16 na kujionea kama matarajio yote yaliyotengenezwa kabla ya tamasha hilo yatageuka kuwa historia mpya ya bendi hiyo kongwe.