Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Si utani! Hebu msikieni Mama Kanumba naye

Muktasari:

  • Mama Kanumba alisema sio kweli kama kifo cha mwanaye ndio chanzo cha kuzorota kwa tasnia hiyo, bali wasanii waliopo wanapaswa kuongeza juhudi katika uigizaji wao ili kufikia mafanikio na hasa wakilenga kutoa kazi zenye ubora na zenye ujumbe kwa jamii.

WALE wanaoendelea kupiga kelele na kuamini marehemu Steven Kanumba ameondoka na filamu Bongo, wamsikilize mama mzazi wa nyota huyo wa zamani, Florence Mtegoa anachokisema, kwani amesema hakuna ukweli wowote katika hilo.

Mama Kanumba alisema sio kweli kama kifo cha mwanaye ndio chanzo cha kuzorota kwa tasnia hiyo, bali wasanii waliopo wanapaswa kuongeza juhudi katika uigizaji wao ili kufikia mafanikio na hasa wakilenga kutoa kazi zenye ubora na zenye ujumbe kwa jamii.

“Tusikate tamaa Kanumba kaondoka yeye, ila sanaa imebaki na watu wasiseme eti filamu zimeondoka na mwanangu, wasanii wajipange na kuandaa kazi nzuri, naamini watarudi pale alipowaachia marehemu Kanumba,” alisema Mama Kanumba.

Juu ya wasanii wanaofananishwa na marehemu mwanae, Mama Kanumba alisema anamuona kijana aitwaye Fred ndiye angalau kidogo anaona anavaa viatu vya Kanumba, japo alisisitiza wasanii wapambane kujifananisha kwa kazi sio mwonekano.