Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shilole: Naishi na bahati yangu 'natoa chuma naweka chuma'

Muktasari:

  • Tukio hilo limefanyika kwenye mgahawa wake wa Shishi Food uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam, wakati akiwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa na pia kutimiza miaka 10 ya biashara hiyo.

MSANII na mjasiriamali, Zuwena Mohamed maarufu Shilole amesema anatoa chuma anaweka chuma na hajali watu wanavyomsema kwamba anavishwa pete za uchumba na kuolewa mara kwa mara baada ya kuvishwa pete na mchumba wake wa sasa, Rich, usiku wa kuamkia leo Desemba 23, 2024.

Tukio hilo limefanyika kwenye mgahawa wake wa Shishi Food uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam, wakati akiwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa na pia kutimiza miaka 10 ya biashara hiyo.

Mwanaspoti ambalo lilikuwapo eneo la tukio, lilimvuta chemba Shilole na kumuuliza suala la kuhusu kuvishwa pete kwa mara nyingine na pia kuzungumzia mipango ya ndoa yake ya nne, alisema: "Kama unavyonijua mimi sina muda wa kupoteza, natoa chuma naweka chuma, wacha watu waseme, kikubwa naishi na bahati yangu ya kuvushwa pete na kufunga ndoa, wapo watu wengine maarufu kama mimi lakini hadi leo hata pete hawajavalishwa, sasa kwanini nisijivunie hili.

"Kwanza niseme tu ukweli sikutegemea hili la kuvalishwa pete usiku huu na Rich, ni jambo la kushukuru kwa kweli, kuhusu matukio ya kuvishwa pete kufanana inapokuwa siku yangu ya kuzaliwa hii niseme tu huwa inatokea tu kwa wahusika kuona zawadi ya kunipatia mimi siku ya bethidei yangu ni pete basi acha tuishi humo, huenda Mungu amenibariki hivyo.

"Kuhusu mipango ya kufunga ndoa, kwasasa nipo tayari kwa ndoa, ni suala la muda tu, tuombe Mungu sababu kuolewa kwa mwanamke ni sunnah, pete imeanza ndoa inafuata."

Katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali, Rich aliongozana na ndugu zake ambao ni mama yake na dada zake. Na ulipofika muda wake, alisogea mbele na kusema anataka kuhalalisha uchumba na Shilole kwa kumvisha pete.

"Habari za saa hizi, kama nilivyotambulishwa, mimi ni shemeji yenu lakini sio wa halali, nimejaribu kufanya 'sapraizi' ingawa Shilole hakuwa anajua hili ila kwa niliposimama hapa nataka kumfanya awe wa halali kwangu kwa kumvalisha pete hii ya uchumba," alisikika akisema Rich kwenye sherehe hiyo.

Kwa upande wa Shilole, baada ya kuvalishwa pete alisema: "Sikutegemea kama Rich atanivisha pete ya uchumba, maana maneno ni mengi, kumbe ananipenda, nimekubali namkaribisha kwenye maisha yangu, nilijua bado ananiangalia angalia tabia," alisema Shilole.

Ikumbukwe kuwa, Shilole amevalishwa pete hiyo baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake Rommy 3D miezi saba iliyopita.

Hii ni pete ya nne ya uchumba kwa Shilole kuvishwa akiwa tayari maarufu, ambapo zipo zilizozaa matunda ya ndoa na nyingine haikuzaa matunda ya ndoa, huku pia kama kama ndoa itafungwa itakuwa ni ya nne kwa Shishi Trump.

Pete ya kwanza Shilole alivalishwa Desemba 20, 2014 na msanii wa bongofleva, Nuh Mziwanda kwenye sherehe ya bethidei ya Shilole, ambapo ndugu jamaa na marafiki wakiwamo wasanii wenzake walihudhuria. Pete hii haikuweza kuzaa matunda ya ndoa kwani wapenzi hao wa zamani waliachana Julai 2015.

Pete ya pili ya uchumba kwa Shilole, alivishwa mwaka 2018 na aliyekuwa mume wake, Ashrafu Uchebe, katika usiku wa harusi yao iliyohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo mashuhuri.

Pete ya tatu ya uchumba kuvalishwa Shilole ilikuwa mwaka 2020 ya Rommy 3D, hii pia alivalishwa siku ya bethidei, ambapo baada ya kuvalishana pete hiyo walikuja kufunga ndoa, lakini ilipofika Mei 28, 2024 ndoa hiyo ilivunjika. Na ya nne ni hii mpya ya Rich.

Kama ndoa hii itafungwa, itakuwa ni ya nne kwa Shishi Baby baada ya awali kuolewa na dereva wa malori akiwa na umri wa miaka 17, ambaye alikuja naye Dar es Salaam kutokea kwao Igunga, ambako alikuwa tayari amepata mtoto wa kwanza. Akazaa mtoto mmoja katika ndoa hiyo, akiwa ni wa pili kwake. Baadaye mwaka 2009 akaachana na mwanaume huyo akimtuhumu kumpiga hadi kumdhuru mguu wake wa kulia.

Ndoa ya pili, Shilole ambaye pia hujiita Shishi Trump, alifunga na Ashraf Uchebe kisha waliachana baada ya awali kuvuja kwa picha zikimuonyesha akiwa amejeruhiwa usoni akituhumu kupigwa na kijana huyo mwenye mwili uliojengeka kimazoezi na kisha akaolewa na mpigapicha wake, Rommy 3D, waliyeachana miezi saba iliyopita.