Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shakira anavyojipigia pesa Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Safari ya Shakira na Kombe la Dunia ilianza 2006  Ujerumani alipotoa burudani kwenye sherehe za kufunga mashindano kupitia wimbo wake maarufu Hips dont lie, hatua iliyomfungulia mlango wa kuwa sura ya muziki wa soka duniani. 

MWANAMUZIKI maarufu wa Colombia, Shakira Isabel, ameendelea kuonyesha kuwa si tu malkia wa muziki, bali pia mmoja wa wasanii waliofanikiwa kuigeuza michuano ya Kombe la Dunia   kuwa chanzo kikubwa cha mapato na umaarufu kwa zaidi ya miaka 20.

Safari ya Shakira na Kombe la Dunia ilianza 2006  Ujerumani alipotoa burudani kwenye sherehe za kufunga mashindano kupitia wimbo wake maarufu Hips dont lie, hatua iliyomfungulia mlango wa kuwa sura ya muziki wa soka duniani. 

Mwaka 2010 ndipo alipopiga bingo kubwa zaidi baada ya FIFA kuuchagua wimbo wake Waka Waka, kuwa wimbo rasmi wa Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini. Wimbo huo uligeuka kuwa moja ya nyimbo zilizofanikiwa zaidi katika historia ya mashindano hayo, ukiendelea kuingiza fedha kupitia majukwaa ya kidijitali hadi leo. 

Mwaka 2014 nchini Brazil alirejea na La La La (Brazil 2014), wimbo uliokuwa sehemu ya albamu rasmi ya Kombe la Dunia kabla ya kutumbuiza kwenye sherehe za kufunga michuano hiyo katika Uwanja wa Maracana. 

Baada ya kukaa nje ya matoleo mawili yaliyofuata, Shakira amerudi kwa kishindo mwaka 2026 kupitia wimbo rasmi wa Kombe la Dunia, Dai Dai, aliouimba sambamba na Burna Boy. Mbali na kuwa wimbo rasmi wa mashindano hayo, pia amepangwa kuongoza burudani katika fainali ya kwanza kabisa ya Kombe la Dunia yenye 'halftime show' maalumu. 

Taarifa za FIFA zinaonyesha kuwa Shakira ni mmoja wa wasanii wachache smwaliowahi kuhusishwa na matoleo manne tofauti ya Kombe la Dunia, jambo linalomfanya kuendelea kuvuna mamilioni ya mashabiki na mapato kupitia mauzo ya muziki, matangazo, mikataba ya kibiashara na haki za matumizi ya nyimbo zake. 

Kana kwamba haitoshi, nyota huyo pia amewaalika wacheza dansi wa Uganda, Ghetto Kids, kushiriki naye katika 'halftime show' ya fainali ya Kombe la Dunia 2026, tukio litakaloongeza zaidi mvuto wa jina lake kwenye jukwaa kubwa zaidi la soka duniani. 

Kwa kifupi, kila Kombe la Dunia linapofika, Shakira anaonekana kuwa miongoni mwa washindi wakubwa hata kabla mpira haujaanza kuchezwa. FIFA inapopata burudani, yeye anapata umaarufu na fedha dili linaloendelea kumlipa kiulaini kwa karibu miongo miwili sasa. 


SOKA LIKAMPA MUME

Mbali na kuvuna mamilioni ya dola kupitia nyimbo za Kombe la Dunia, Shakira pia alipata Mume kupitia soka, staa wa zamani wa Barcelona na Manchester United, nyota wa Hispania, Gerard Piqué, aliyekuwa sehemu ya video hiyo.

Penzi lao lilichanua sambamba na mafanikio ya Hispania iliyotwaa ubingwa wa dunia mwaka huo. Wawili hao walidumu pamoja  na kupata watoto wawili kabla ya kuachana 2022.

Ni kama vile Kombe la Dunia limekuwa na faida kubwa kwa Shakira tena kwa wakati mmoja, umaarufu, fedha na mapenzi. Ingawa penzi na Pique lilifika mwisho, biashara yake na FIFA imeendelea kushamiri hadi leo, huku akirejea tena mwaka 2026 kama mmoja wa nyota wakubwa wa burudani za michuano hiyo.