Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kombe la Dunia limemkumbatia Shakira

Muktasari:

  • Jambo hilo linamfanya achukuliwe kama "Malkia wa Nyimbo za Kombe la Dunia' safari yake  ya kutumbuiza katika ufunguzi wa Kombe la Dunia ilianza tangu 2006 nchini Ujerumani.

INGAWA  sio mchezaji wa soka, jina la Shakira litabaki kuwa alama katika historia ya mashindano ya Kombe la Dunia  kwa  sauti na vionjo  katika fainali za Kombe la Dunia.

Jambo hilo linamfanya achukuliwe kama "Malkia wa Nyimbo za Kombe la Dunia' safari yake  ya kutumbuiza katika ufunguzi wa Kombe la Dunia ilianza tangu 2006 nchini Ujerumani.

Mwaka 2006 katika fainali za Ujerumani, Shakira hakuwa na wimbo rasmi, lakini aliweka rekodi ya baada ya kutumbuiza wimbo wake maarufu Hips Don’t Lie (Bamboo Remix) katika sherehe za kufunga mashindano hayo jijini Berlin.

Supastaa huyo raia wa Colombia alitua 2010 na wimbo wa Waka Waka  (This Time for Africa) ulioteuliwa kuwa wimbo rasmi wa Kombe la Dunia  ambao ulimpa heshima kubwa baada ya kutumbuiza katika sherehe za ufunguzi na kufunga.

Malkia huyo  aliyezaliwa Februari 2, 1977 pia alipata nafasi 2014 aliporejea Brazil na wimbo wake wa La La La uliokuwa sehemu ya kampeni ya muziki ya FIFA.

Hata hivyo kihistoria unaonyesha kuwa wimbo rasmi wa mwaka huo ulikuwa We Are One (Ole Ola) ulioimbwa na Pitbull akishirikiana na Jennifer Lopez na Claudia Leitte.

Mwaka 2018 na  2022 nchini  Russia na Qatar mtawalia Shakira hakutoa wimbo mpya mahsusi wa mashindano. Hata hivyo nyimbo zake za nyuma hasa Waka Waka ziliendelea kutumika katika matangazo na video za mashabiki, zikithibitisha kuwa ushawishi wake hauchuji licha ya kutokuwa na kazi mpya.

Mwaka huu amrpata nafasi nyingine tena ya kutumbuiza wimbo mpya uitwao Dai Dai akimshirikisha staa wa Nigeria, Burna Boy, hivyo ni kati ya wanamuziki wakubwa wenye bahati ya kupafomu katika michuano mikubwa hiyo.