Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Selena Gomez: Binti mavumba

Selena Gomez

Muktasari:

Selena Marie Gomez alizaliwa Julai 22, 1992, Grand Prairie, Texas, Marekani na akiwa ndio kwanza ana umri wa miaka 22 anatajwa kuwa miongoni mwa wasanii wanaoingiza fedha nyingi duniani.

MWITE mavumba au binti mahela, hiyo ni kutokana na ukweli kwamba unapowazungumzia wasanii mabinti wa umri mdogo wenye fedha duniani huwezi kuwa na sababu ya kumuweka kando Selena Gomez.

Selena Marie Gomez alizaliwa Julai 22, 1992, Grand Prairie, Texas, Marekani na akiwa ndio kwanza ana umri wa miaka 22 anatajwa kuwa miongoni mwa wasanii wanaoingiza fedha nyingi duniani.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, hadi mapema mwaka jana inadaiwa kwamba Selena aliyewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Justin Bieber alikuwa na kipato kinachozidi Pauni 16 milioni.

Mbele ya wengi anafahamika katika uigizaji filamu na uimbaji na utunzi wa nyimbo, fani hizo mbili ndizo zilizomuwezesha kuupata utajiri ambao leo hii umempa heshima ya kipekee akimiliki magari ya bei mbaya na kuishi maisha ya kifahari.

Pamoja na utajiri, Selena ametokea mbali, baba yake Ricardo Joel Gomez na mama yake Amanda Dawn “Mandy” aliyekuwa mpambaji kumbi kabla ya maonyesho waliachana akiwa na miaka mitano tu.

Wakati Selena anazaliwa mama yake alikuwa na miaka 16 tu huku akiwa ametawaliwa na umasikini na ugumu wa malezi na hivyo kulazimika kufanya kazi zaidi ya moja ili kumudu maisha.

Selena amekuwa akimsifia mama yake kwa namna alivyojitolea kwa ajili yake na wakati akiwa katika kupanga majukwaa, Selena naye alitumia fursa hiyo hiyo kudhihirisha kipaji chake katika uigizaji.

Akiwa na miaka saba alishiriki mfululizo wa filamu ya watoto ya Barney and Friends akitumia jina la Gianna, kwa mara ya kwanza alionekana katika toleo la saba na nane la filamu hiyo.

Akikumbuka zama hizo, Selena anasema kwamba alipata tabu kwani alikuwa akiona aibu lakini anasema huo ulikuwa mwanzo mzuri, alijifunza mengi hadi leo hii amekuwa kati ya waigizaji tishio.

Alianza kupanda chati mwaka 2006 aliposhiriki mfululizo wa filamu ya Wizards of Waverly Place iliyoanza kuonyeshwa Marekani kuanzia mwaka 2007 hadi 2012.

Filamu hiyo iliyotwaa tuzo mbalimbali ndiyo iliyokuwa sababu ya Selena na mama yake kuhamia Hollywood lakini hapo hapo akarekodi wimbo wa “Everything is Not What It Seems” uliosaidia kutangaza kipaji chake cha uimbaji.

Akiwa na miaka 19 umahiri wake katika muziki ulianza kulipa, kwa onyesho moja Selena alikuwa akilipwa Dola 100,000 na zaidi. Kati ya nyimbo zake nyimbo wimbo mmojawapo iliomtangaza vizuri ni ule wa Love You Like a Love Song”.

Selena aliishtua dunia kwa jeuri ya fedha mwaka 2012 akiwa ndio kwanza binti mwenye miaka 20 alipotoa Dola 2.17 milioni ili kununua jumba la kifahari lililokuwa mali ya mkali wa filamu, Jonah Hill. Jumba hilo lenye vikorombwezo vyote ikiwamo sehemu ya kuchezea mpira wa kikapu na bwawa la kuogelea lipo Tarzana, California.

Hata hivyo habari za hivi karibuni zinadai kwamba Selena amelipiga bei jumba hilo kwa Dola 3.45 milioni na waliolinunua ni mkali wa kikapu wa Marekani, Nick Young na mpenzi wake rapa Iggy Azalea.

Nje ya utajiri huo, Selena ni mtu mwenye kupenda kufanya manunuzi (shopping) kwa fujo ingawa pia yupo mstari wa mbele katika kutoa misaada ya kijamii.