Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rumba la Tanzania halikuanzia Kongo

Muktasari:

  • kweli inatokana na jinsi ambavyo kwa miaka mingi bendi za Tanzania zimekuwa zikiiga upigaji wa muziki wa rumba kutoka kwa wanamuziki wa Kongo. Lakini kuna ushahidi wa kihistoria unaopingana na dhana hii.

Watu wengi huwa wanaamini kabisa kuwa wanamuziki  wa Tanzania walijifunza muziki wa rhumba kutoka Kongo, hii kwa kweli inatokana na jinsi ambavyo kwa miaka mingi bendi za Tanzania zimekuwa zikiiga upigaji wa muziki wa rumba kutoka kwa wanamuziki wa Kongo. Lakini kuna ushahidi wa kihistoria unaopingana na dhana hii.

Katika moja ya santuri zilizorekodiwa na mwanamuziki Adam Salim Malya akiwa na kundi lake aliloliita The Adam Salim Trio, mwishoni mwa miaka ya 40, ulikuwemo wimbo ulioitwa Rumba Leo.

Huyu Adam Salim Malya ambaye ni Mchaga kama linavyoonekana jina lake, ndiye mtunzi halisi wa wimbo maarufu wa Malaika ambao hujulikana zaidi kama ni utunzi wa Fadhili William kutoka Kenya, lakini hiyo ni mada ya siku nyingine.

Utunzi huu wa Adam Salim na pia historia ya mwanamuziki Salum Abdallah kutoka Morogoro, ambaye1942 alianzisha bendi aliyoipa jina la La Paloma. La Paloma lilikuwa ni jina la wimbo maarufu uliotungwa na Mhispaniola aliyeitwa Sebastian Iradier mwaka 1850.

Wimbo huu ulikuja kuwa maarufu duniani kote, na hata zama hizi bendi nyingi bado zinaupiga wimbo huo majukwaani, japokuwa kwa hakika wanamuziki Wachache sana wanaojua historia ndefu ya wimbo huu.

Mwaka 1944, Salum Abdallah alitoroka kwao Morogoro na kuelekea Mombasa, nia yake ni kuwa apande meli na kwenda Cuba kujifunza muziki wa Rumba. Muziki wa Rumba uliingia Afrika kupitia santuri za muziki wa Cuba zilizokuwa zikijulikana kwa namba zilizoanzia GV. La Paloma ulikuwa GV 103. 

Santuri hizi kutoka Cuba ndio zilizochochea upenzi wa mitindo kama rumba, cha borelo na kadhalika kwa wapenzi wa muziki wa Afrika ikiwemo nchi yetu. Safari ya Salum Abdallah kwa bahati mbaya aliipanga bila kujua madhara ya vita ya pili ya dunia iliyokuwa ikiendelea wakati huo, hivyo akaishia kukwama Mombasa.

Wakati huo Kongo ilikuwa haijaanza kutoa santuri zake. Ukisikiliza muziki wa bendi zilizokuweko Tanganyika kati ya mwaka 1920 na 1930 kama vile Dar es Salaam Social Orchestra na YMCA Social Orchestra, na vikundi vingine vilivyokuweko zama hizo, mitindo yao ilikuwa ikiiga mipigo ya rumba kutoka Cuba, Kongo haikujulikana kabisa.

Kongo ilianza kutoa santuri zake mwaka 1947, na mwaka 1953 ndipo Joseph Kabasele maarufu kama Grand Kale ambaye hujulikana kama baba ya muziki wa Kongo alipounda bendi yake ya African Jazz.

Kabasele alileta mabadiliko makubwa katika upigaji wa muziki wa rumba huko kwao na umahiri wake ulienea sehemu kubwa Afrika, kwa mfano mwanamuziki maarufu marehemu Manu Dibango alitoka kwao Cameroon na kuhamia Kongo kwa muda mrefu, ambako alijiunga African Jazz kuongeza ujuzi wa upigaji wa saksafon uliokuja kumfanya ajulikane duniani.

African Jazz ya Joseph Kabaselle ilitoa nyimbo zake zilizokuwa na mpangilio  mzuri wa magitaa matatu, saksafon na trampet na tumba, na uimbaji wa kuvutia wa Tabu Ley na Joseph Kabasele, na baada ya nyimbo hizi kurekodiwa na kusambazwa zikaanza kuingia Afrika ya Mashariki na ndipo bendi za hapa kwetu na Afrika Mashariki kwa ujumla, zikaanza kuiga kila mtindo uliokuwa ukitoka Kongo, na hivyo kueneza imani kuwa wanamuziki wa Tanzania walijifunza muziki kutoka Kongo.

Ubunifu wa wanamuziki wa Kongo ulikuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka. Dr Nico alipoacha bendi ya African Jazz, na kuunda African Fiesta, alihama na kaka yake Dechaud, huyu ndiye husifika kwa kubuni wazo la kuwa na gitaa la nne katika muziki gitaa hili liliitwa ‘mi solo’ au maarufu kwa jina la ‘second solo’. 

Ukisikiliza nyimbo za African Fiesta utasikia gitaa la Dr Nico likiongoza muziki lakini likisindikizwa na magitaa mawili, gitaa la rhythm na gitaa la mi solo lililokuwa likipigwa kwa ufundi na kaka yake.

Baada ya hapo asilimia kubwa ya bendi zilianza kutumia mi solo na kila bendi ikaweka ubunifu wake tofauti katika kutumia gitaa hili. Bendi zetu nazo nyingi zikawa zinatumia mtindo wa kupiga pia gitaa la mi solo. 

Franco akiwa na OK Jazz alifanya mabadiliko makubwa katika rumba la Kongo, akawa na upigaji wake wa gitaa kwa mtindo wa ‘kent’, ambao ulikuwa ni aina fulani ya upangaji vidole wakati wa kupiga gitaa. Mtindo huu nao ukaigwa sana na wapiga magitaa maarufu huku kwetu kama vile Mbaraka Mwinyshehe, Hamza Kalala na Patrick Balisidya.

Wapiga gitaa la rhythm kutoka Kongo kama vile Vata Mombasa wa Lipua Lipua na Lele Nsundi wa Orchestra Kiam, wakaja na mtindo mpya wa ufungaji wa nyuzi katika magitaa yao. Gitaa huwa lina nyuzi sita zenye unene tofauti na hupewa majina ya uzi wa kwanza mpaka wa sita , uzi wa kwanza ukiwa ndio ule mwembamba. 

Hawa akina jamaa wakawa hawautumii uzi wanne, badala yake pale kwenye nafasi ya uzi wa nne wakawa wafunga uzi wa kwanza na kuleta sauti tamu sana walipokuwa wakipiga gitaa hilo. Mtindo huo ukafuatwa na bendi nyingi za hapa kwetu.

Tarehe 22 mpaka 24 Septemba 1974, katika jiji la Kinshasa kulifanyika tamasha la muziki lililoitwa Zaire 74, wanamuziki maarufu Marekani kama James Brown, BB King na Bill Withers walishiriki, onyesho hili lilifanya wanamuziki wa Kongo wapate darasa lililowasaidia kubuni aina nyingine ya muziki na bendi kama Orchestra Sosoliso zikaja na ubunifu wake katika uchezaji na upigaji uliotohotelewa kwenye upigaji wa muziki wa soul, upigaji huo mpya nao ulikuja tena kuigwa na bendi zetu. Vijana Jazz Band waliiga sana Orchestra Sosoliso na kuanzisha mtindo wao waliokuwa wakiuita Koka Koka Balaa. TP OK Jazz wakabuni tena staili mpya ambapo walianza kupiga magitaa mawili ya solo katika wimbo mmoja. 

TP Ok Jazz walimpata Mavatiku Visi Michelino, mpiga solo mahiri kutoka bendi ya Afrisa ya Tabu Ley, mwanamuziki huyu ambaye asili yake ni Angola kama alivyokuwa Sam Mangwana, alichukuliwa na TP OK Jazz kuwa mpiga solo. Mavatiku akawa anapiga solo, wakati huohuo Franco naye akipiga solo katika wimbo huohuo mmoja, staili hii ya upigaji wa solo mbili ndiyo iliyotumika na bendi ya TP OK Jazz mpaka bendi hiyo ilipopotea kwenye anga za muziki.

Bendi ya OK Jazz ilipokuja Tanzania, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nje ya Kongo baada ya kifo cha Franco, , ilitumia vyombo vya Vijana Jazz Band, na Vijana Jazz Band wakati huo ikiwa na wapiga magitaa mahiri, Shaban ‘Wanted’ Yohana, Shaaban Dogodogo, Agrey Ndumbalo, Manitu Musa, na Baker Semhando waliiga style hii ya kupiga magitaa mawili ya solo na kutumia kwenye nyimbo kama
VIP na Thereza zilizokuwa utunzi wa marehemu Jerry Nashon na kwenye wimbo Mfitini na Malaine zilizokuwa tungo za John Kitime