Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo aachana na demu wake

Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo na mrembo mwanamitindo kutoka Russia, Irina Shayk. Picha na Maktaba

Muktasari:

“Tunaweza kuthibitisha kwamba Irina Shayk amehitimisha rasmi uhusiano wake na Cristiano Ronaldo,” ilisema taarifa.

SASA ni rasmi kwamba penzi la Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo na mrembo mwanamitindo kutoka Russia, Irina Shayk limekufa.

Kwa mujibu wa wakala wa Irina, penzi hilo maarufu zaidi katika soka kwa sasa limekufa.

“Tunaweza kuthibitisha kwamba Irina Shayk amehitimisha rasmi uhusiano wake na Cristiano Ronaldo,” ilisema taarifa.

Bado haijajulikana sababu hasa ya kuvunjika kwa uhusiano huo ambao awali ulionekana kuwa imara, lakini wakati huohuo wakala huyo amekanusha uvumi kwamba penzi hilo limevunjika kutokana na uhusiano mbovu kati ya Irina na mama yake Ronaldo.

“Irina amekuwa na uhusiano mzuri na familia ya Ronaldo katika kipindi chote cha uhusiano wao. Habari zozote hasi kuhusu Irina na familia ya Ronaldo ni uongo,” ilisema taaifa hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Ureno, inadaiwa kuwa Irina aligoma kuhudhuria sherehe za mama yake Ronaldo kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa. Inadaiwa kuwa Irina alimwambia wazi Ronaldo kwamba asingehudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mama huyo iliyofanyika katika Visiwa vya Madeira Ureno ambako ndipo anakotoka staa huyo.

Kutokana na kauli hiyo, nyota hao waliingia katika mgogoro ambao mwishowe ulihitimisha uhusiano wao ambao umedumu kwa miaka mitano na kulikuwa na ubashiri kwamba huenda Ronaldo angemuoa mrembo huyo.

Kuonyesha kuwa wawili hao walikuwa wameachana, Irina hakuhudhuria tuzo za Mwanasoka Bora wa Dunia wakati Ronaldo alipoitwaa tuzo hiyo wiki iliyopita. Vilevile Irina aliacha kuufuatilia ukurasa wa Twitter wa Ronaldo.

“Cristiano alikuwa amepanga kumfanyia ‘Surprise’ mama yake kwa sababu alikuwa Dubai na Irina katika Krismasi, alikuwa amepanga kwenda ghafla katika sherehe hiyo lakini Irina hakutaka kwenda,” alisema mtoa taarifa mmoja.

“Walibishana sana na mwishowe iiishia kwa Ronaldo kusheherekea Mwaka Mpya akiwa na mwanaye tu. Irina alikasirika na kubwatuka kuhusu Dolores (mama yake Ronaldo) lakini Ronaldo aliamua kuwa katika upande wa mama yake.”

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, inadaiwa kuwa hivi karibuni Irina aliamua kubaki hotelini baada ya Dolores kuwa katika nyumba ya Ronaldo mitaa ya La Finca.

“Dolores anaamini kuwa Irina siyo mwanamke mwafaka kwa Ronaldo. Alitaka Ronaldo awe na mwanamke ambaye anaamini kwa siku za mbele atachukua jukumu la kuwa mama wa kumtunza mtoto wa Ronaldo, Cristiano Jr. hicho hakikuwa kipaumbele cha Irina.”

Mama huyo ndiye anayemtunza zaidi mtoto wa Ronaldo ambaye mama yake mzazi hajulikani na inadaiwa kuwa amelipwa pesa nyingi kumzalia Ronaldo na kukaa zake kimya.

Kuonyesha kuwa uhusiano baina ya wawili hao umekufa, Ronaldo hakulitaja jina la Irina katika hotuba yake ya kushukuru mara baada ya kuteuliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Dunia. Ilikuwa ni tofauti na alipolitaja jina hilo katika tuzo za mwaka 2014.

“Ni kipindi kisichosahaulika katika maisha yangu kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia kwa mara ya tatu. Najisikia furaha sana kupokea tuzo hii na nataka kujipa changamoto mwenyewe kila siku. Inabidi niishukuru familia yangu, watu wote walionisapoti Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno ambao wananifanya niwe bora kila siku,” alisema Ronaldo siku aliyopokea tuzo bila ya kumtaja Irina.

Taarifa ya awali iliyotolewa na watu wa habari wa Irina ni kwamba mrembo huyo hakuhudhuria sherehe hizo kwa sababu alikuwa na kazi nyingine.

Hata hivyo, wengi walihoji kukosekana kwake kwa kutokana na sababu hiyo duni kwa sababu kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita ilishajulikana kuwa Ronaldo angekuwemo katika orodha ya wachezaji watatu ambao wangewania tuzo hiyo.

Uvumi kuwa wawili hao wameachana ulizidi baada ya Irina kutompongeza Ronaldo baada ya kuchaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Dunia.

Badala ya kumpongeza Ronaldo, Irina aliamua kuposti picha zake zikimuonyesha akiwa likizo sehemu akisheherekea kutimiza miaka 29. Katika picha hizo pia hakukuwa na dalili ya kuonekana kwa Ronaldo.