Rayvanny ambwaga Diamond Afrimma, Zuchu naye noma

Bosi wa Next Level Music, Rayvanny ameshinda tuzo ya AFRIMMA 2022 kipengele cha msanii bora wa kiume Afrika Mashariki.

Tuzo hizo ambazo zimetolewa usiku wa kuamkia leo nchini Marekani, Rayvanny baada ya kupokea tuzo hiyo amesema ilikuwa ndoto yake siku moja kuipata.
Katika kipengele hicho Rayvanny amewabwaga wasanii John Frog (South Sudan), Khaligraph Jones, Otile Brown (Kenya), Eddy Kenzo (Uganda), Diamond Platnumz  (Tanzania), na Meddy (Rwanda).
Pia kipengele cha msanii bora wa kike Afrika Mashariki imeenda kwa staa Zuchu kutoka lebo ya WCB akiwapiku Femi One (Kenya), Jovial (Kenya), Nandy (Tanzania), Winnie Wagi (Uganda), Maua Sama (Tanzania), Sanapei (Kenya), Sheeba Karungi (Uganda).
Ikumbukwe Rayvanny ndio msanii pekee kutoka Tanzania anayemiliki tuzo ya BET aliyoshinda 2017 katika kipengele cha Viewers Choice Best New International Act Artist.