Rayvann na WCB! kama sio sasa basi baadae

PALE Wasafi Classic Baby (WCB) kuna wasanii kibao ambao wanasumbua kinoma kwenye muziki kwa sasa, lakini kuna kichwa kimoja kina vipaji kibao kinaitwa Rayvann.
Dogo amejaaliwa kipaji cha kuimba, kutunga na cha kukupa mzuka zaidi ni kwamba, anaimba, anarap na anajua kuzungusha mauno yaani ni mkali pia wa jukwaani.
Pale WCB, Rayvann pamoja na udogo wake lakini anaonekana kuwa na nyota ya kuja kuwa mfalme fulani hivi kwenye game ya Bongo Flava, yaani wazee wa kuweka mkeka wenyewe wanasema kama sio sasa hivi basi baadaye kidogo tu.
Sasa Rayvann amepiga stori mbili tatu na Mwanaspoti na kufunguka mambo kibao, ambayo hakika ulikuwa huyafahamu kabisa na kama unayojua, basi ni kwa juu juu tu.
Yaani huna zile za ndani kabisa ambazo ndio tamu na za motooo.
Anaingia kwenye muziki
Kama ilivyo kwa mastaa wengi wa muziki ambao wanasumbua kimataifa kwa sasa, Rayvann pia alianza muziki baada ya kipaji chake kuibuliwa kanisani kwenye kwaya ambako, wengi wanapatia mzuka huko.
“Nilianza kwa kuandika kwa mashairi, nikaingia kurap kisha kuimba kwa sababu nimeimba sana kanisani ambako nilifundishwa namna ya kupanga sauti. Baada ya hapo nilianza kuandika ngoma za kuimba, tulikuwa watu kama sita na wote tulianza kuimba kanisani. Si unajua kuna mambo ya kwaya, hivyo siku tumeingia kanisani tukajiunga na kwaya ya kanisa.”
Anasema wakiwa kanisani ndipo wakajijenga vizuri na baadaye akageukia muziki. Alishiriki mashindano ya kufanya free style wakati huo akiwa shuleni.
“Niliposhiriki mashindano ya free style, kuna mtu alinisikia nikiimba, akasema wewe upo vizuri zaidi kwenye kuimba. Basi niliendelea kurap nikashinda kimkoa, baadaye tukashindanishwa Tanzania nzima nikashinda nikawa namba moja, kwakweli sikujua kama muziki una pesa. Niliposhinda nikapewa mtonyo na hapo sikutaka kulaza damu,” anasema Rayvann, ambaye alitua na kupikwa kwenye Kundi la Tip Top Connection kabla ya kutua Wasafi.
VIPI KWA DIAMOND
Kwa sasa nyota ya Rayvann inawaka kwelikweli kwani, mpaka sasa ndiye msanii ambaye amefanya ngoma nyingi na Diamond ndani ya WCB.
Wamefanya wote ngoma ya Salome, Zilipendwa, Fresh ambayo pia ndani kuna sauti ya Fid Q kisha Iyena ambayo Zari amekula shavu kama Video Queen.
Lakini, kitu ambacho ukifahamu ni kuwa, mpenzi wake Rayvann yaani ule utamu wake uleee, amekuwa akipiga naye kazi bega kwa bega unaambiwa. Iko hivi. Rayvanny anakula bata na mrembo, Fahyma ambaye wana mtoto mmoja kwa sasa, ametokea kwenye video tatu.
Kwanza Fahyma alionekana kwenye ngoma ya Kwetu, ambayo ilimtambulisha vyema Rayvann kwenye gemu ya Bongo Flava, kisha akachomoza kwenye ngoma ya Natafuta Kiki, Safari ambayo amemshirikisha Nikki wa Pili na baadaye akauza sura kwenye Siri.
Bifu na Hamornize
Ukikaa na maswahiba na watu wa karibu na WCB wanakwambia kuna bifu la chini kwa chini baina ya Rayvann na Harmonize japo wenyewe wamekuwa wakiyeyusha kinoma.
Kinachoelewa ni kwamba, bosi wa WCB, Diamond amekuwa karibu sana na Hamornize kuliko wengine, jambo ambalo linaonekana kama linawavuruga chini kwa chini.
“Kwanza Diamond hana upendeleo kwa wasanii wake na hilo tunashukuru sana na hakuna bifu na Hamornize labda watu wanachukulia tofauti. Tuko karibu sana na mara nyingi naposti kitu kisha Harmonize anakomenti na namjibu shit ndio watu wanahisi hivyo, lakini hiyo ni staili yetu na tumezoeana sana,” alisema.
ANAMKUBALI KING KIBA
Bila kupepesa macho wala kubana koo lake, Rayvann anafunguka kuwa anapenda kazi za Ali Kiba, ambaye ni hasimu wa bosi wake, Diamond.
Amefunguka kuwa kati ya wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa nchini, Ali Kiba ni mmoja wapo na yuko tayari kufanya naye kolabo bila ya tatizo.
“Wasanii wanaofanya vizuri nchini wako wengi ukiacha Diamond, pia yupo Ali Kiba, namkubali sana jamaa kwa kazi zake.