PUMZI YA MOTO: Wasanii wetu wanaiga hata haya?

KUUZA roho katika ulimwengu wa Kiswahili sio msemo maarufu, lakini huko Magharibi hasa Marekani ni msemo wa kawaida.

Wenyewe wanaita selling the soul to the devil au making deal with the devil. Maana ya jumla ya msemo huu ni kitendo cha mtu kufanya njia za haramu hasa kutumia nguvu za giza ili kutimiza malengo; utajiri, umaarufu, madaraka na kadhalika.

Watu wengi maarufu wa Magharibi hasa wasanii wakubwa huhusishwa na mambo haya. Mfano halisi ni wimbo wa Eminem wa Sold my Soul wa mwaka 2022. “I sold my soul to the devil. I’m going to hell. I’m headed to hell. I want the money, the women, the fortune, and the fame. That Means I’ll end up burning in hell scorching in flames. Satan’ll be in to see me later to see if I’m interested in being partners. Devil worshippin’, Satan music.”

“Niliuza roho yangu kwa shetani. Ninaenda jehanamu. Ninaelekea jehanamu. Nataka hela, wanawake, mali na umaarufu. Hii maana yake nitaishia kuungua moto wa jehanamu. Shetani naye atakuwepo kuniona na baadaye kuona kama nimevutiwa kuwa mweza wake. Kuabudu mashetani. Muziki wa kishetani.”

Dalili za wasanii wa aina hii huwa ni matendo ya ajabu ajabu wanayoyafanya hasa wanapokuwa kwenye kazi zao. Hapa ndipo paliponifanya nijiulize kwa nyota wetu wa muziki wanavyofanya wakati mwingine huwa ni ajabu sana. Nyota hawa huvaa nguo za michoro ya mafuvu ya binadamu moja ya alama za wauza roho. Kwenye tamasha fulani  karibuni ilikuwa balaa. Kuna nyota mmoja alivaa maguo yenye michoro ya maskeletoni (masalia ya mifupa ya mwili wa binadamu). Hizi ndizo dalili kuu za wauza roho wa Magharibi. Nitatumia ukurasa wa mitandao ya kijamii ya Instagram na Tiktok wa youwontbelievemeofficial kama mfano.

Ukurasa huu umekuwa ukichambua matukio yanayoashiria imani hii kwenye kazi za wasanii wanaohusishwa kuanzia mashairi, video hadi matamasha. Ukurasa huo ukaenda mbali zaidi na kutafuta mahojiano nao na kukiri kwa ndimi zao kujihusisha na mambo hayo.


HOPSIN NA ISHARA YA MPINGA KRISTO

Agosti 26, mwaka huu, Rappa Hopsin (pichani juu) alifanya tamasha huko Colorado Springs na kupitia skrini kubwa ya projekta iliyokuwa ikitumika kupamba tamasha lake ikaonyeshwa picha ya kishetani ya Mpinga Kristo.

Japo yeye mwenyewe baadaye aliomba radhi akisema hakujua lolote kuhusu picha hiyo, lakini ukweli ni kwamba kuna asilimia kubwa jambo hilo lilipangwa kwa makusudi huku akijua. Picha hiyo ya kishetani ilionyeshwa wakati akiimba wimbo wa Ill Mind of Hopsin 7’.”

Huu ni wimbo ambao msanii huyo amezungumzia kutokuwa kwake na Imani ya dini.

Hopsin ambaye jina lake halisi ni Marcus, anasema “Now I’m dealin’ with this backlash because Marcus isn’t a Christian Sasa napambana na hiki kimbembe kwa sababu Marcus sio mkristu

Is Heaven real? Is it fake? Is it really how I fantasize it?

Mbinguni kupo kweli? Au ni uongo? Ni kweli ninavyoichukulia?

Where’s the Holy Ghost at? How long’s it take a man to find it?

Roho mtakatifu yuko wapi? Itachukua muda binadamu kumpata?

You gave me the Bible and expect me not to analyze it?!

Mmenipa Biblia na kutarajia sitoichambua?

I’m not readin’ that motherfuckin’ book, because a human wrote it.

Sikisomi hicho kitabu cha hovyo kwa sababu binadamu ndiyo amekiandika.


NB

Mtu kama huyu akisema picha ya Mpinga Kristu iliwekwa bila yeye kujua, utamuamini?


KUPITIA            VIDEO ZAO

Nyuma ya wasanii hawa kuna kampuni kubwa ambazo lengo lake ni kupotosha dunia.

Kampuni hizi hutumia pesa nyingi kutengeneza video za kishetani na kuzifanyia promosheni kubwa, kama video ya mwanadada Doja Kat. Kwenye video ya wimbo wake mpya wa Demons (majini), mwadada huyo katumia picha za kutisha zenye kudhirisha kwamba AMEUZA ROHO yake.

Halafu kwenye mashairi yake, anasema How my demons look (How them demons)

Now that my pockets full? (Ayy, ayy, ayy, yeah, ayy)

Majini yangu yanaonekanaje?

Sasa ni kwamba mfuko wangu umejaa

I am on to bigger things

I just bought a limousine (A limousine)

You live like me in your dreams (Yes, you do

Nafanya mambo makubwa.

Nimenunua Limousine

Unaishi maisha yangu kwenye ndoto zako


NB

Doja Kat anaonyesha kwamba kupitia majini, yakiwakilisha imani za kuuza roho ametoboa na anaishi maisha mazuri akiendesha magari kama Limousine.


KUPITIA MASHAIRI YAO

Drake - msanii kutoka Canada

Katika moja ya mahojiano yake ambayo yamepostiwa kwenye ukurasa huo, anasema kazi yake ya sanaa inaongozwa na nguvu ambayo hata yeye mwenyewe haijui.

I can use all my heart and my soul, in my writing but at the end of the day, I am being guided by some other power. I don’t know what it is.

Naweza kutumia moyo watu wote na roho yangu yote, katika kuandika kwangu (mashairi), lakini mwisho wa siku huwa naongozwa na na baadhi ya nguvu ambayo sijui ni nini!

Haya ni maneno mazito sana na yenye kufikirisha. Drake anaizungumzia nguvu fulani kutoka kusikokulikana ikiongoza kazi zake.

Yaani yeye anaandika mashairi halafu anashangaa kazi zake zinakuwa kubwa mno...hajui hiyo inatoka wapi.

Lakini ukitaka kufahamu inakotoka nguvu hiyo, sikiliza baadhi ya mashairi yake kutoka nyimbo mbalimbali, alizoimba mwenyewe au kwa kushirikishwa.


1. Do not disturb

I am a reflection of all of your insecurities

Behind closed doors, a lot of 6 God worshipping

Mimi ni kielelezo ca matatizo yako yote.

Kisirisiri, ibada nyingi sana za miungu sita.


2. Sneaking

This is all God’s doin’, man, you can’t plan it

But if the devil’s in the details, then I’m Satanic

Haya yote anafanya Mungu, mtu, huwezi kupanga.

Lakini kama ya kishetani yapo kiundani, basi mimi wa kishetani.


3. Madiba Riddim

Devil’s working overtime

Voodoo spells put on my life

Shetani anafanya kazi kwa muda wa ziada

Uchawi umetapakazwa maishani mwangu


4. Gold Roses feat Rick Ross)

Roxx’ll do you filthy for me soon as I give him the nod

Meanin’ he’ll blast for me like puttin’ the 6 with the God

Roxx atakufanyia balaa kwa niaba yangu muda si mrefu nikimruhuru

Ninamaanisha atalipuka kwa niaba yangu kama kuiweka 6 na Mungu.


5. 6 God

I’m the real 6 God boy

I’m about to say a true thing


Mimi ni kijana halisi wa Mungu wa SITA

Nakaribia kusema UKWELI.


6. Meltdown (alioshirikishwa na Travis Scott)

But the truth is you scared of the SIX

Lakini ukweli ni kwamba unatishika na SITA


7. When to say When

Six God praying hands like I am religious man

But I am just a sicker man, wicked man

Mikono ya Mungu SITA ni kama mimi ni mtu wa dini. Kimbe ni mtu wa hovyo, ni mtu muovu.


NB

Mjumuisho wa yote hayo, Drake kairudia rudia sana namba 6, ambayo ni ishara kuu ya ushetani (666).

    Vijana wetu wamekuwa wakifanya vitu vingi sana kwa jamii na sanaa kwa jumla. Wanaitangaza sana Tanzania kimataifa, hilo halina ubishi. 

   Lakini haya matendo ya kupitia mavazi, matamasha na video zao yanatia shaka.Vijana wameuza roho?