Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Prisca Lyimo afunguka mazito kuhusu Iyabo Ojo, soko la Nigeria

PRISCA Pict

Muktasari:

  • Kwenye tahmthilia hiyo iliyojaa mastaa kibao wa Nollywood, Prisca ni miongoni wa watanzania walioigiza kwenye tamthilia hiyo wakiwemo pia Jux, Zuchu, Othman Njaidi.

MWANAMITINDO na muigizaji wa Tanzania, Prisca Lyimo amesema hakutarajia kupokelewa kwa upendo Nigeria na hilo limebadilisha mtazamo wake kwenye maisha na sanaa kwa jumla.

Ikumbukwe Prisca hivi karibuni alikuwa Nigeria kwenye uzinduzi wa tamthilia ya ‘The Return of Arinzo’ iliyoandaliwa na muigizaji maarufu wa nchini humo, Iyabo Ojo.

Kwenye tahmthilia hiyo iliyojaa mastaa kibao wa Nollywood, Prisca ni miongoni wa watanzania walioigiza kwenye tamthilia hiyo wakiwemo pia Jux, Zuchu, Othman Njaidi.

Akizungumza na vyombo vya habari, Prisca alieleza namna alivyopokelewa vizuri na mwanamitindo Priscilla Mkambala pamoja na mama yake Iyabo Ojo akisema nje ya kazi wamekuwa na ukaribu mkubwa.

“Lakini ukweli ni walinipokea kama familia tangu siku ya kwanza na hilo lilinifanya nijisikie nipo nyumbani,” alisema Prisca

Aliongeza Priscilla ambaye pia ameigiza kwenye tamthilia hiyo hakumchukulia kama mshindani wake alimfanya ajihisi kamandugu wa damu.

Akimzungumzia Iyabo ambaye ni mama mkwe wa msanii wa Bongo Fleva, Juma Jux alisema “Alinitazama kama mtoto wake na sio mgeni alinipa heshima, alinilinda na alinifanya nijihisi nipo nyumbani.”

“Lakini ni mtu anayejali kazi yake yaani anafanya kwa utaratibu na ndio maana Iyabo anafanikiwa kutokana na kuwajali kila msanii na kuthamini kazi yake.”

Prisca, ambaye amewahi kuonekana kwenye tamthilia kama Jua Kali, Jacobs Daughters na Tufani hii ni mara yake ya kwanza kuigiza tamthilia nje ya Tanzania.

Uwepo wa mwanadada huyo kwenye tamthilia hiyo inaelezwa ni mojawapo ya njia ya kujitangaza kimataifa kupitia sanaa yake kutokana na soko la Nigeria.

Mbali na uigizaji Prisca aliwahi kuwa mshindi wa tatu kwenye mashindano ya kutafuta warembo la Miss Tanzania mwaka 2020, nafasi ya pili ilichukuliwa na Juliana Rwehimiza mshindi alikuwa Rosey Manfere.