Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Njaidi anavyotembea na Kanumba kimataifa

NJAIDI Pict

Muktasari:

  • Miongoni mwa wanaoyaendeleza maono hayo ni Othman Njaidi maarufu Patrick Kanumba, anayechukuliwa kama mmoja wa vijana wanaotamani kuendeleza ndoto na mwelekeo aliouacha Kanumba.

SAFARI ya ndoto huanza na mtu mwenye maono na muda mwingine huziendeleza mwenyewe au huja kumalizia wengine.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa marehemu Steven Kanumba, ambaye licha ya kufariki dunia mwaka 2012, alikiacha kiwanda cha Bongo Movie kwenye harakati za mageuzi.

Kanumba alikuwa mmoja wa waigizaji kuitangaza filamu ya Tanzania kuvuka mipaka hususan Afrika Magharibi kama Nigeria ambako tasnia hiyo imeendelea kwa kasi.

Miongoni mwa wanaoyaendeleza maono hayo ni Othman Njaidi maarufu Patrick Kanumba, anayechukuliwa kama mmoja wa vijana wanaotamani kuendeleza ndoto na mwelekeo aliouacha Kanumba.

Njaidi, ambaye alitambulishwa katika tasnia hiyo na Kanumba mwenyewe kupitia filamu kama ‘This is It’ (2010), ‘Uncle JJ’ na nyinginezo anaonekana kupiga hatua kubwa sio tu ndani ya Tanzania, bali pia kimataifa.

NJAI 01

NDOTO YA KIMATAIFA

Enzi za uhai wake, Kanumba alikuwa na matamanio makubwa ya kuifikisha Bongo Movie kimataifa.

Kanumba alikuwa akisisitiza umuhimu wa wasanii wa Tanzania kufikiria soko la nje ili kuinua zaidi sekta hiyo.

Aliamini kuwa ubora wa kazi za Bongo Movie unaweza kushindana na tasnia nyingine kubwa barani Afrika, hususan Nollywood ya Nigeria.

NJAI 05

Katika mahojiano mbalimbali, alieleza dhamira yake ya kushirikiana na wasanii wa kimataifa na kusambaza filamu zake nje ya mipaka ya Tanzania kwani awali aliwahi kufanya kazi na Wanigeria, Mercy Johnson na Noah Ramsey. Mwaka 2011 Kanumba na Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ walikwenda Ghana kurekodi filamu mpya iliyowakutanisha mastaa wengine wa Afrika lakini wakati wakiwa kwenye harakati za kuiachia mwaka 2012 akafariki.

Kwenye mahojiano enzi ya uhai wake “Nimefurahia sana kufika hapa nchini Ghana kwa ajili ya kurekodi sehemu ya filamu hii, ni mara yangu ya pili kutumia vifaa vikubwa katika tasnia hii, mara ya kwanza ilikuwa wakati narekodi tangazo la Zantel,” alisema Kanumba.

“Hawa jamaa wamejiandaa si mchezo, kumbuka timu nzima ya watayarishaji imetoka Hollywood. Filamu hiyo itaanza kurekodiwa rasmi Machi mwakani 2012, kwa sasa tunarekodi sehemu tu ya utambulisho.”

NJAI 02

NJAIDI ANAKUJA

Enzi za Kanumba, Njaidi na Jenipher aliokuwa anaigiza nao walikuwa kwenye kiwango bora na maarufu nchini.

Na hata baada ya kifo chake wasanii hao wameendelea kufanya kazi zao taratibu lakini sasa ni kama Njaidi anaanza kufuata ndoto yake kimataifa.

Hatua kubwa zaidi ni ushiriki wake katika tamthilia mpya ya ‘The Return of Arinzo’, kazi inayowaunganisha wasanii kutoka mataifa mbalimbali ikiwamo Nigeria. Tamthilia hiyo inayoongozwa na muigizaji maarufu wa Nigeria, Iyabo Ojo na imekusanya majina makubwa ya tasnia ya Nollywood akiwemo mke wa msanii wa Bongofleva, Juma Jux.

NJAI 04

Katika tamthilia hiyo inayotarajiwa kuachiwa hivi karibuni wapo mastaa kutoka Tanzania akiwemo Jux, Zuchu, Njaidi na Prisca Lyimo anayechipukia katika soko.

Kuwepo kwa Njaidi katika kazi hiyo si jambo dogo. Ni ishara kuwa uwezo wake unatambuliwa nje ya Tanzania, jambo ambalo sio rahisi kulifikia kwa wasanii wengi wa ndani.

“Kwanza niwashauri vijana wenzangu wenye vipaji tutumie mitandao ya kijamii kama njia ya kujitangaza kwa sababu hata mimi waliona kazi zangu kupitia mitandao basi wakasema huyu ndiye mtu tunayemhitaji ndio nikapata dili hilo.”

Wadau wanaona kuwa hatua hiyo ni mwendelezo wa kile ambacho Kanumba alitamani kuona wasanii wa Tanzania wakifanya kazi bega kwa bega na nyota wa kimataifa.

NJAI 03

JUX KIUNGANISHI

Mbali na juhudi binafsi za Njaidi, kuna mchango wa mahusiano katika kufanikisha kazi hiyo.

Jux ambaye ni mkwe wa Iyabo na familia yake akiwemo dada yake Fatma Mkambala alipendekeza Njaidi kuwepo kwenye tamthilia hiyo.

Anasema: “Jux namfahamu muda mrefu ni shabiki yangu namba moja hivyo ilivyotokea dili hilo yeye na dada yake Fatma Mkambala hawakusita kunipendekeza hivyo wana mchango mkubwa wa mimi kuwa kwenye tamthilia hiyo. Thamani imepanda na nimepata koneksheni kubwa kwa sababu tunakutana na watu tofauti na Nigeria wametupokea vizuri sana.”