Pole ya Nandy yamfurahisha Mimi mars

NGOMA ya Mimi Mars iitwayo Pole aliyomshirikisha Nandy imempa furaha mwanadada huyo anayefanya vyema pia kwenye tamthilia ya Jua Kali, akisema hivyo ndivyo inavyotakiwa kwake kwenye sanaa hiyo.
Bidada huyo damu moja na Vanessa Mdee, amesema hakutarajia kama ngoma hiyo ingepokewa vyema kutokana na ukweli ni muda mrefu aliukaushia muziki na kujikita zaidi kwenye uigizaji.
“Sanaa inanihitaji nami naihitaji zaidi ukubwa nilioonyeshwa na mashabiki wangu unanifanya nijione nahitajika kwenye muziki na kuigiza hivyo kazi iliyobaki ni kufanya kazi kwa bidii ili kuwapa furaha mashabiki wangu,” alisema Mimi Mars.
“Pole umekuwa wimbo mkubwa kwangu umepokewa vizuri na mashabiki na nimepokea maoni mengi kuwa sanaa inanihitaji natakiwa kufanya kazi kwa bidii ili niwatumikie mashabiki wa sehemu zote,” alisema.
Mimi Mars alisema anapenda kuigiza na kuimba hivyo ni jukumu lake kuhakikisha anafunika kote.