P Funk atema nyongo sakata la Paula

Monday April 19 2021
majani pic
By Nasra Abdallah

Paul Matthysse maarufu P Funk Majani ambaye ni  mzazi mwenzie na Kajala Masanja, amefunguka kwa mara ya kwanza  tangu kutokea kwa sakata linalowahusisha Paula na Kajala na kueleza kuwa linaichafua hata familia yake.

Majani amezungumza hayo leo Aprili 19, 2021 alipohojiwa na kituo cha redio Clouds katika kipindi cha XXL.

Sakata hilo liliibuka kwa mara ya kwanza Februari 14, 2021 kwa Rayvanny kuweka video zikimuonyesha akiwa na Paula katika mahaba mazito ndani ya gari.

Hata hivyo wiki iliyopita kukavuja meseji nyingine zinazodaiwa ni za Harmonize alikuwa akimtumia Paula ambazo zilionyesha ni watu walio katika mahusino.

Matukio yote haya yalisababisha wasanii hao kufikishana Polisi, lakini kipindi chote hicho Majani hajawahi kuzungumza lolote kuhusiana na sakata hilo mpaka leo alipoamua kutema nyongo.

Katika maelezo yake, Majani ambaye ni mtayarishaji wa muziki wa siku nyingi amesema ”Kwa sababu nimeshawaambia mwaka jana kuwa mimi nimeshajitoa, mtu ushajitoa, usha 'give up' basi ndio hivyohivyo

Advertisement

“Kwa sababu mtoto anatafuta laana, alishaniambaiaga wewe mimi sio baba yangu, basi ibaki hivyohivyo, umenielewa eeeh na Kajala sio familia yangu na bahati mbaya nimezaa na mama ambaye sio sahihi hafai kuitwa hata mama,hanihusu kwa ufupi kwa  sasa,” ameeleza Majani.

Ameenda mbali na kubainisha kuwa “Mtu akishakuambia wee sio baba yangu, utamng’ang’aniza, mimi nina familia yangu nyingine ambayo lazima nisimame kama baba nihakikishe wapate mazingira mazuri, malezi mazuri.

“Pia hivi vitu wanavyofanya hawa ndugu zetu huko vinaathiri hata hawa kwa sababu wanachukulia ooh wadogo zake fulani hata shuleni wapi sijui kama umeisoma, ule uchafu waliofanya unareflect kwa hawa wengine ambapo sio vema ni kosa kubwa, wametuvunjia sana  heshima hawa watu" amesema Majani

Ameongeza kuwa “Ngoja nikuambie kitu la msingi, jibu sahihi  maisha sio Instagram,  sehemu ya kutatua shida za kifamilia sio social media, sijui kuna mjinga ukisoma anasema toa tamko, nitoe tamko wee kama nani, wee ni nani nikutolee tamko, tamko limeanza Instagram.

“Huwa vitu vya kifamilia unatakiwa ukae na wazee,  waliosababisha mazingira sio, wale ndio mnaka chini kifamilia, sio kuweka weka kwenye mitandao kwenye vyombo vya habari  na hao pia ni wapuuzi waliovujisha hizo video sio sahihi hivyo vitu," amesema P Funk.


Advertisement