Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Odama hatishwi na yeyote yule

Odama Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Odama alisema kwa jinsi anavyoweza kuulinda ustaa alionao kwa kutengeneza kazi nzuri zinazohitajika kwa walaji sokoni, haoni wa kumtisha kwa sasa.

MWIGIZAJI mkongwe wa filamu Bongo aliye pia mtayarishaji wa tasnia hiyo, Jennifer Kyaka ‘Odama amedai kuwa hakuna staa yeyote wa sasa anayempa changamoto wala kumtisha kwenye fani hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Odama alisema kwa jinsi anavyoweza kuulinda ustaa alionao kwa kutengeneza kazi nzuri zinazohitajika kwa walaji sokoni, haoni wa kumtisha kwa sasa.

“Nina miaka 20 katika hili gemu, sina changamoto yoyote inayoweza kunisumbua kutoka kwa mastaa wa sasa, lakini naweza kuwaambia wafanye kazi kwa bidii, fani hii ili udumu ni lazima kila mmoja ajitoe kwa hali na mali kuhakikisha anatoa kazi nzuri zitakazolipa sokoni,” alisema Odama anayemiliki kampuni ya kuzalisha filamu ya J-Film 4life inayochuana na kampuni nyingine katika fani hiyo.

Mwanadada huyo ameanika sababu ya kuamua kufungua kampuni yake kuwa, ilikuwa ni ndoto na lengo la  kuwa mjasiriamali, huku akishukuru kampuni hiyo kuzalisha filamu na tamthilia zinazofanya vyema katika runinga za ndani na nje ya nchi.