Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nay wa Mitego afunguka siri nzito za mademu wa kibantu

Muktasari:

  • Anapoachia ngoma yake mpya mashabiki hutikisikia. Wala haihitaji maneno mengi, ni kama vile alipoachia ‘Muziki Gani’, ‘Nakula Ujana’, ‘Akadumba’, ‘True Boy’ na ‘Salamu Zao’.

NAY wa Mitego, ndio ni mmoja kati ya majina maarufu katika tasnia ya Bongo Fleva kutokana na kuachia kazi kali zinazowashika watu hadi wakashikika.

Anapoachia ngoma yake mpya mashabiki hutikisikia. Wala haihitaji maneno mengi, ni kama vile alipoachia ‘Muziki Gani’, ‘Nakula Ujana’, ‘Akadumba’, ‘True Boy’ na ‘Salamu Zao’.

Ni kutokana na ukali wa ngoma zake na ule mvuto alionao kwa mashabiki, ndipo Mwanaspoti lilipoamua kufanya mahojiano na msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Elibariki kuhusiana na muziki pamoja na maisha kwa ufupi. Ni kutokana na ‘ubize’ alionao wa kudili na mistari studio, mahojiano haya yalifanyika kwa njia ya simu.

Mwananspoti: Haloo! Habari yako Nay.

Nay wa Mitego: Poa, nani mwenzangu?

Mwanaspoti: Naitwa Rhobi.

Nay wa Mitego: Ohooo Sorry, unajua nilipoteza simu, vipi uko poa?

Mwanaspoti: Niko poa kabisa, vipi, mbona upo kimya kwenye muziki?

Nay wa Mitego: Siko kimya, sema nimeamua kufikiri kuhusu kutunga nyimbo. Maana nimekuwa nikitumia tasfida katika muziki wangu kila mara, lakini kitu kinachonikosesha amani ni kwamba watu wanafumbua tasfida na yanakuwa maneno ya kawaida, mara ya mwisho nimetoa wimbo wa ‘Mikono juu’ ulio tofauti na nyimbo zangu zilizopita, lakini nilishangaa ukaingia katika orodha ya kufungiwa.

Mwanaspoti: Katika video zako umekuwa ukiwatumia zaidi warembo wenye maumbo makubwa ya Kibantu, ni kwanini?

Nay wa Mitego: Unajua ukimweka mwanamke mwenye umbo la kuvutia katika video, watu wanapenda. Fuatilia video zote zilizofanya vizuri duniani utagundua ndani yake kuna wasichana, hiyo ndiyo sababu inayofanya na mimi niwatumie kwenye video zangu.

Mwanaspoti: Umekuwa haudumu na mwanamke katika mapenzi, kwa nini huwa inakutokea hivyo?

Nay wa Mitego: Hahaa! Hilo mbona ni jambo la kawaida, nafikiri kwa sababu nikiwa na mtu naanika wazi uhusiano, hivyo nikiachana naye watu wanajua, labda ndiyo maana unahisi hivyo.

Mwanaspoti: Kwanini unapenda kuvaa mlegezo wakati wewe ni kioo cha jamii?

Nay wa Mitego: Kwenye mlegezo daah! Napenda tu, maana nimeanza kuvaa hivi tangu nikiwa darasa la tatu. Lakini watu waangalie kazi zangu na sio mlegezo.

Mwanaspoti: Msanii gani unayemkubali Bongo?

Naywa Mitego: Kuna wengi ninaowakubali wakiwamo Juma Nature, Mr. Blue ambao walikuwa wananiumiza kichwa tangu kitambo hicho, pia Diamond namkubali sana.

Mwanaspoti: Jina la Nay limetokana na nini?

Nay Mitego: Hilo nilipewa na demu wangu wa Kihindi akimaanisha ‘Hapana’ kutokana na ugumu wa maisha niliokuwa nao.

Mwanaspoti: Umekuwa mtu wa matukio mengi,ni tukio gani ambalo huwezi kulisahau?

Nay wa Mitego: Siwezi kusahau siku nilipozungumza tena na mama yangu. Nilikaa miaka mitano bila kuongea na mama, shida ilikuwa ni haya mambo ya ujana, lakini yaliisha na mama akanipa baraka za kuendelea kufanya muziki.

Mwanaspoti: Machi 25 mwaka jana ulikamatwa na polisi ukiwa Morogoro ikiwa ni siku chache baada ya kutoa wimbo ‘Wapo’, vipi ulifanya nini mara tu baada ya kukamatwa?

Nay wa Mitego: Kwanza nilipogundua polisi wameizunguka hoteli niliyokuwa nimelala, nilimpigia simu mama kumtaarifu, nikamwambia atulie, awe na amani.

Mwanaspoti: Nashukuru sana kwa ushirikiano Nay.

Nay wa Mitego: Asante sana, nitakuja ofisini kwenu kuwatembelea

Mwanaspoti: Karibu sana.