Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nani kutwaa tuzo za BET leo?

Muktasari:

Nani kutwaa tuzo za BET leo? Hilo ndilo swali wanalojiuliza wafuatiliaji wa tuzo za Black Entertainment Television (BET).

Nani kutwaa tuzo za BET leo? Hilo ndilo swali wanalojiuliza wafuatiliaji wa tuzo za Black Entertainment Television (BET).

Tuzo hizo zilizoanza kutolewa mwaka 2001 ni mahususi kwa ajili ya kusherehekea mafanikio ya kazi za Wamarekani weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji na michezo, zinatarajiwa kutolewa usiku wa leo huko nchini Marekani.

Kwa nchi za Africa wasanii wanaotazamwa zaidi katika tuzo hizo ni Diamond Platnumz akiwa mwakilishi pekee kutoka Tanzania, Burna Boy na Wizkid wote kutoka nchini Nigeria ambao hawa mwaka jana tayari waliweka historia ya kutwaa tuzo kubwa za Grammy.

Wasanii hawa kwa pamoja wanachuana katika kipengele cha

Best International Act’.

Wengine wanaoshindanishwa nao ni Aya Nakamura (Ufaransa),Emicida (Brazili), Headie One (Marekani) Young T & Bugsey (Marekani) na Youssoupha (Ufaransa)

Macho yanatolewa zaidi kwa Burna Boy na Diamond,baada ya hivi karibuni kuibuka kampeni za kuwapigia kura wasanii hao licha ya kuwa utaratibu wa BET haupo hivyo na badala yake kazi hiyo kufanywa na majaji maalum walioteuliwa kwa shughuli hiyo.

Ni kutokana na hilo hata wasanii wa Bongo na Afrika Mashariki kwa ujumla walijikuta wakijigawa wengine wakimtetea Diamond Platnumz ambaye alikuwa akishambuliwa na baadhi ya watu kuwa sio msanii anayesimama kwenye matatizo na wananchi.

Huku wengine wakisema anapaswa kuungwa mkono kutokana na kuufikisha muziki wa BongoFleva mbali na amekuwa msanii mfano kwa vijana wengi wanaotoka familia za kimasikini.

Endapo Diamond atashinda,hii itakuwa mara yake ya kwanza kwani katika tzo hizo alishatajwa zaidi ya mara mbili lakini akaangukia pua.

Wakati Burna Boy yeye akishinda hii itakuwa mara yake ya tatu,kwani alishashinda tena katika kipengele hicho mwaka 2019 na 2020 .

Huku Wizkid yeye alishinda mwaka 2012 baada ya kipengele hicho  kugawanywa kwa upande wa Marekani na Afrika na mwaka  2020 alishinda kipengele cha BET HER kupitia wimbo wa  'Brown Skin Girl' alioshirikishwa na Beyonce.

Tayari wasanii hao wameshawasili Marekani jana kwa ajili ya shughuli hiyo.