Nandy avunja ukimya kuachana na Bilnass

Tuesday May 11 2021
nandy pic
By Nasra Abdallah

Msanii wa muziki wa Bongofleva, Nandy amevunja ukimya kuhusu tetesi za kuachana na mpenzi wake Bilnass.

Ukimya huo kauvunja leo Jumanne Mei 11, 2021 alipokuwa anazindua msimu wa pili wa tamasha lake la Nandy Festival.

Nandy ambaye jina lake halisi ni Faustina Mfinanga, amesema  maneno yanayosemwa kuhusu kuachana na mpenzi wake huyo watu wayapuuze kwani hakuna mahali wenyewe wameshatoka mbele na kusema wameachana.

Wakati kuhusu ushiriki wake kwenye Nandy Festival inayoanza kurindima Juni 6 mkoani Kigoma, amesema Billnas atakuwepo kwani ni moja ya watu ambao tamasha hilo linamuhitaji.

"Bilnass ni msanii mkubwa ni product ambayo Nandy Festival inamuhitaji sana, hivyo watu wategemee kwamba atakuwepo katika tamasha letu," amesema Nandy

Amesema jumla ya mikoa saba tamasha hilo litarindima huku Mkoa wa Kigoma ukiwa wa kwanza kufungua, na mikoa miwili itakuwa ya Kenya ambayo ni Nairobi na Mombasa.

Advertisement
Advertisement