Mwigizaji Freddy afariki dunia akipatiwa matibabu Mloganzila

Muktasari:
- Taarifa hiyo imethibitishwa na mwigizaji mwenzie Blandina Changula 'Johari' wakati akizungumza na Mwanaspoti
Mwigizaji wa Bongo Movie Freddy Kiluswa amefariki dunia leo Novemba 16,2024 akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mloganzila.
Taarifa hiyo imethibitishwa na mwigizaji mwenzie Blandina Changula 'Johari' wakati akizungumza na Mwananchi
"Siwezi hata kuongea chochote, lakini taarifa za kifo ni kweli amefariki leo akiwa anapatiwa matibabu hospitali Mloganzila, "amesema Johari ambaye alikuwa mzalishaji wa tamthilia ya 'Lawama' ambayo Freddy amewahi kucheza