MUSIC FACTS: Rich Mavoko kampa shavu Mbosso WCB Wasafi

ANAJIITA Messi wa Bongofleva kutokana na ukali wa uimbaji, uandishi na uchezaji wake jukwaani. Ameshatengeneza ngoma kubwa za kutosha na anahesabika miongoni mwa waimbaji wazuri Tanzania. Rich Mavoko, mtoto wa Mama Richard ameshatoa albamu na EP. Amefanya kolabo za kimataifa, kwa kifupi ana historia yake ndani ya Bongofleva. Bongo Music Facts inakuja zaidi;


1. Kabla ya Rich Mavoko kusaini WCB Wasafi hakuwahi kukutana au kuongea na Diamond Platnumz kuhusu hilo, AY ndiye aliyemkutanisha na Sallam SK wakiwa nchini Uganda kwenye shoo ya Jose Chameleone ndipo yalipoanza mazungumzo ya kujiunga.

2. Verse ya mwisho ya wimbo wa Malaika, Rarua imeandikwa na Rich Mavoko, ndio ngoma iliyofanya vizuri hadi Malaika kupata tour

Washington DC, Marekani mwaka 2017.

3. Lulu Diva alimlipa Rich Mavoko fedha ili kumshirikisha katika wimbo wake ‘Ona’ licha ya kudaiwa ni wapenzi, video ya wimbo huo ndio video ya pekee ya Lulu Diva iliyofikisha views zaidi ya milioni 1 YouTube.

4. Wimbo namba tisa kutoka kwenye albamu ya Diamond Platumz ‘A Boy From Tandale’ uitwao ‘Sijaona’ umeandika na Rich Mavoko wakati huo yupo chini ya WCB Wasafi.

5. Licha ya kutokea Morogoro, Rich Mavoko hajawahi kuutaja mkoa huo katika nyimbo zake kama wasanii wengine, hii ni sawa na Wizkid ambaye hajawahi kutaja jina hilo katika ngoma zake, anatumia zaidi jina la Starboy.

6. Video za nyimbo zote ambazo Rich Mavoko alizitoa chini ya WCB Wasafi kama ‘Kokoro’, ‘Rudi’ na ‘Imebaki Stori’ zimeondolewa kwenye majukwaa ya kidijitali kama YouTube.

7. Rich Mavoko hapendi kutoka ‘out’ na msichana ambaye wakifika sehemu ya kula bata ataanza kujidai anajuana na kila mtu. Hiyo ni sawa na Mwana FA ambaye huwa hapendi kukaa na msichana mwenye kelele akiwa viwanja.

8. Fid Q ndiye msanii wa Hip Hop Bongo aliyefanya kolabo nyingi zaidi na Rich Mavoko. Hadi sasa wawili hao wameachia ngoma kama ‘Sheri’, ‘Blow Up’, ‘Tawile’, ‘Champion’ na ‘Bambam’.

9. Kama sio muziki Rich Mavoko basi angekuwa mcheza soka, shuleni alicheza pamoja na mchezaji wa Azam FC, Frank Domayo, Mavoko alicheza namba nane ili kutokana na ufupi wake Mwalimu akamuhamishia namba saba.

10. Rich Mavoko ndiye alienda nyumbani kwa Mbosso na kumchukua hadi Sinza zilipokuwepo ofisi za WCB Wasafi kwa wakati huo na ndipo siku hiyo Mbosso alisaini mkataba wa kuwa chini ya lebo hiyo. Mbosso alikuwa ameshakata tamaa ya muziki ila Mavoko alikuwa anamtia moyo kila walipokuwa wanakutana katika mazoezi ya mpira.