Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msiba wa Jengua wawaibua mashabiki Yanga

Aliyekuwa muigizaji wa filamu nchini Mohamed Fungafunga amezikwa leo Desemba 16 jijini Dar es Salaam katika makaburi ya Mianzini yaliyopo Mburahati.

Sasa kwa sababu enzi za uhai wake mzee huyo alikuwa shabiki wa Yanga iende irudi, katika mazishi yake walihudhuria mashabiki maarufu wa Yanga yaani Mark Yanga na Mzee Vigeregere.

Akimzungumzia mzee huyo Mark amesema kwake anamfananisha mzee huyo na straika wa Yanga, Saido Ntabazonkiza.

"Tuko hapa kwa sababu mbili. Kwanza mzee alikuwa mwananchi mwenzentu. Lakini pia tunaukubali sana uwezo wake wa kuigiza. Tunaweza kumfanisha na uwezo wa Ntabazonkiza kwenye soka," amesema Mark.

Ntibazonkiza ni mshambuliaji mpya wa Yanga ambaye ameonekana kuanza na makali kwenye kikosi hicho cha Wananchi baada ya kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United.

Wawili hao walitinga msibani wakiwa ndani ya uzi wa nyumbani wa Yanga huku Mark akiwa amevalia kama anavyoovaaga akiwa majukwaani jezi ya rangi ya njano na miwani kubwa.

Jengua alifariki jana akiwa nyumbani kwa mwanae kwenye matibabu huko Mkuranga Pwani ambapo inaelezwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na presha.