Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mnyama: Acheni kulipua ngoma

Muktasari:

  • TID, ambaye ametesa na ngoma kibao ikiwemo Zeze, amesema nyimbo za sasa hazidumu muda mrefu kwa sasa kwa kuwa, zinalipuliwa tu na kuandikwa kwa wepesi.

TID a.k.a Mnyama ameamua kufunguka mzima mzima unaambiwa na kuwachana livu wasanii wanaochipukia kwa sasa.

TID, ambaye ametesa na ngoma kibao ikiwemo Zeze, amesema nyimbo za sasa hazidumu muda mrefu kwa sasa kwa kuwa, zinalipuliwa tu na kuandikwa kwa wepesi.

Tofauti na ngoma za wasanii wa zamani, ambazo zilikuwa zikiandaliwa kwa umakini na msanii hutumia muda mrefu kujipanga.

“Nyimbo nyingi za zamani tulikuwa tunatumia muda kuandika, pia waandaji wanafanya ‘mixing’ vizuri tofauti na ngoma za siku hizi zina copy kutoka nje ndio maana hazidumu,” TID aliliambia Mwanaspoti.

TID amesema wasanii wanatakiwa kuacha kukopo nyimbo za nje ili muziki wa Tanzania uendelee kukuwa na sio kuishia tu nchini kwetu.