Mke wa Messi kambloki Suzy Cortez sababu ya mumewe

Muktasari:
Cortez amekuwa akimfuatilia Messi kwa miaka mingi na mara si moja amekuwa akijitia uchizi kwa kuposti picha za kizushi za kama vile kumtega staa huyo.
MKE wa Lionel messi amelazimika kum-bloki kichuna mwanamitindo maarufu kutoka Brazil, Suzy Cortez kwenye mitandao ya kijamii kutokana na tabia zake kwa mumewe.
Juzi kati Cortez aliyewahi kuwa mshindi wa Shindano la Makalio ‘Miss Bum Bum’, aliendelea kuonyesha jinsi anavyomzimikia Messi safari hii akichora tattoo ya nyota huyo kwenye kalio lake.
Tattoo aliyoichora ni jina lake Messi, nambari ya jezi yake 10 na logo ya Barcelona, Cortez kwenye kalio lake la kushoto.
Levo hizi zimemfanya mke wa Messi Antonella Roccuzzo kumblok kwenye mitandao ya kijamii kuhakikisha anagalau hafikii dume lake ambalo amepata nalo watoto watatu.
Alipohojiwa, alisema alifanya hivyo kwa sababu anaamini Messi atashinda tuzo yake ya sita ya Ballon d’Or mwaka ujao na hivyo aliifanya kama heshima.
Cortez amekuwa akimfuatilia Messi kwa miaka mingi na mara si moja amekuwa akijitia uchizi kwa kuposti picha za kizushi za kama vile kumtega staa huyo.
Kichuna huyo aliyetwaa ubingwa wa Miss Bum Bum 2015 shindano la makalio yenye mvuto Brazil, aliwahi kuvua nguo na kuuchora mwili wake mzima na rangi za jezi ya Messi. Kitu hicho amefanya mara mbili.
Pia, mara kwa mara ameonekana akiishabikia Taifa la Argentina kwa sababu ya Messi licha yake kuwa anatokea Brazil moja ya mataifa bora kwenye ulimwengu wa kandanda.