Mchekeshaji Mr Ibu akatwa mguu kuokoa maisha yake

Mchekeshaji nguli wa Nigeria, John Okafor ‘Mr IBU’ amekatwa mguu jana baada ya kufanyiwa upasuaji mara saba na sasa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi 'ICU'.
Taarifa iliyopostiwa na binti yake kwenye ukurasa wake wa Instagram imewomba Wanigeria wote wamuombee dua mbali na kumchangia fedha za matibabu.
"Kufikia saa saba mchana jana, baba yangu amefanyiwa upasuaji mara saba, hata hivyo ili kuokoa maisha yake na kuongeza uwezekano wake wa kupona, ilibidi mguu mmoja ukatwe.”
“Tukio hili limekuwa gumu kwetu sote lakini imetubidi tukubali ukweli huu mpya wa hali ya baba ili kumuweka hai.''
Mr IBU alianza kuugua tangu mwezi Oktoba mwaka huu na alionekana katika video moja akiwa amelazwa hospitalini, akiomba msaada wa kifedha.