Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo matatu ya Amini kwenye muziki

AMINI

HERIETH MAKWETTA AMINI, ambaye anatamba na wimbo wa 'Unikimbie' anasema ana nguzo kuu tatu ambazo anazitekeleza katika maandalizi ya kazi yake ndio maana inawavutia mashabiki wengi wanaofuatilia kazi yake. "Kabla sijatunga wimbo wowote ninakuwa makini katika kuhakikisha nimetuliza kichwa changu kwani ninakuwa nimetenga muda muafaka wa kuifanya kazi ipasavyo," anasema Amini ambaye ni miongoni mwa wasanii chipukizi wanaong'ara kwa sasa. Jambo la kwanza anasema kuwa nakiamini anachokifikiria na hicho ndicho anakifanyia kazi kwani kwa kuwa na `melody' nzuri ndiko kunakomfanya azidi kujizolea mashabiki. "Ninahakikisha nakuwa makini ninapoutengeneza wimbo wangu na baada ya kumaliza ninarudia mwanzo mpaka mwisho kwa usahihi na baada ya hapo ninahakikisha vibwagizo ya wimbo wangu imekaa sawa," anasema Amini. Kitu cha pili ni namna anavyoweza kuandaa; "Maneno mazuri ndio msingi bora wa kufanya wimbo ukubalike kwa mashabiki." Hata hivyo Amini anaeleza kuwa nguzo yake ya tatu anahakikisha anafuata misingi yote ya uimbaji, na hilo ndilo lililomfanya afike alipo. "Nipo makini katika kufuata misingi ya uimbaji kwani ninajua namna ya kupanda na kushuka ninapotengeneza wimbo na ninahakikisha sitoki nje ya biti." Amini anafafanua kuwa ametoka mbali na anazidi kukua taratibu na kujifunza mengi katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya na hiyo inamsaidia kujijenga vizuri. Albamu ya pamoja aliyoifanya na Barnabas ndiyo iliyoweza kumweka juu msanii huyo na sasa anaandaa albamu ya peke yake ambayo tayari ameshaanza kuitengeneza. "Nilitoka na Barnabas kwa awamu ya kwanza kwa sababu kila mmoja alifahamika kwa nafasi yake lakini hivi sasa nimeshaanza kuandaa albamu yangu mwenyewe. Ninatumia muda mwingi hivi sasa katika kuandaa albamu yangu ambayo nitaikamilisha mwanzoni mwa mwaka 2011," anasema Amini. 'Kumanya', 'Tumetoka Mbali', 'Anavuruga', 'Subira', 'Mapenzi ya Nani Duniani' na 'Unikimbie' aliyofanya katika studio ya Ngoma Record ni baadhi ya nyimbo zitakazokuwepo kwenye albamu hiyo.