Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo 10 wasiofahamu rafiki zako kuhusu Lady Jaydee

LEO kupitia Bongo Music Facts nakusogezea mambo 10 ya kawaida ambayo rafiki zako wameshindwa kuyafahamu kumhusu Lady Jadee ambaye amerekodi nyimbo zaidi ya 170, huku akifanya kolabo zaidi ya 100.


1. Wimbo wa kwanza wa Lady Jaydee ulirekodiwa MJ Records na Prodyuza Master J. wimbo huo unakwenda kwa jina la Sema Unachokata, alikuja kuurudia tena na ukauwekwa kwenye albamu iitwayo Asubuhi iliyotoka mwaka 2000 ikiwa na nyimbo za wasanii wengine.

Nafasi ya kurekodi MJ Records aliipata baada ya kushinda kwenye shindano la kuimba la kipindi cha DJ Show cha Radio One, nyimbo zilizompa ushindi ni Keep On wa Mc Lyte, Stranded wa Lutricia McNeal na Gotta Get You Home wa Foxy Brown.


2. Lady Jaydee amewahi kuwaandikia wasanii kadhaa nyimbo. Wasanii hao ni kama Nakaya Sumari, Keisha, Patricia Hillary na Papii Kocha pia Jide ameandikiwa mistari ya verse ya kwanza ya wimbo wake I Miss You na Rapa One The Incredible.


3. Lady Jaydee ni miongoni mwa wasanii walioshiriki kwenye wimbo wa maombolezo ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1999.

Ni wakati akiwa bado ni Mtangazaji wa Clouds FM kwani taaluma pekee aliyosomea ni uandishi wa Habari katika Chuo cha Times School of Journalism (TSJ).


4. Msanii wa Raggae toka Jamaica, Luciano hakuweza kutokea kwenye video ya wimbo wa Jide, Anaweza iliyotoka Machi 2018, ni kitu ambacho na Jide amewahi kufanya kwenye wimbo wa Bode uitwao Kama Hunitaki ulitoka zaidi ya miaka 17 iliyopita.


5. Huyu ndiye msanii wa kike wa Bongofleva anayeongoza kutoa albamu nyingi zaidi akiwa nazo nane, albamu yake ya kwanza ni Machozi ambayo ilitoka mwaka 2000 na yote ilirekodiwa MJ Records.


6. Mistari yote Lady Jaydee aliyoimba kwenye wimbo wa Profesa Jay uitwao Nimeamini ameandikiwa na Jay mwenyewe. Jide aliweza kuchana kwenye wimbo huo kutokana na kuwa mwanzoni alikuwa rapa.


7. Lady Jaydee huwa hapendi kusaini mikataba ya kusimamiwa kimuziki, huu ni ushauri aliopewa na Gwiji wa muziki Afrika toka Zimbabwe, Oliver Mtukudzi aliyefariki Januari 23, 2019.


8. Tangu Lady Jaydee kuanza muziki ameshinda na kutunukiwa tuzo zaidi ya 35, ukijumlisha tuzo za Tanzania na zile za kimataifa ambapo ameshinda kwa miaka 15 mfululizo.


9. Rihanna ndiye msanii wa kike duniani ambaye anamvutia Jide kwa sasa baada ya kizazi cha kina Whitney Houston aliyefariki Februari 11, 2012 - anataja kinachomvutia zaidi kutoka kwa Rihanna ni melody.


10. Jide ndiye msanii wa kwanza wa Bongofleva kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro, Uhuru Peak hapo Januari 2013 na hadi sasa hakuna msanii wa kike aliyefanya hivyo, huku Mwana FA akiwa msanii pili Oktoba 2019.

Alijigharamikia kila kitu pekee na alivyofanya hivyo kwa mapenzi binafsi, hii ni baada ya kuimba chorus ya wimbo wa Joh Makini na G Nako uitwao Kilimanjaro.