Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo 10 wasiofahamu rafiki zako kuhusu AY

MWENYEWE anakiri kuwa wimbo wake, Ni Raha Tu ndio uliomtoa kimuziki. Huyu ni AY ambaye amekuwepo kwa kitambo kirefu akitoa burudani na kujipachika majina kama Mzee wa Commercial, Zee, The Butcher na mengine kibao.

Kutokana na uzito wa jina lake, Bongo Music Facts haina budi kukueleza mambo 10 wasiyofahamu rafiki zako kuhusu AY ambaye ni bosi wa Unity Entertainment iliyowahi kuwasimamia wasanii kama Ommy Dimpoz na Stereo.


1. Prodyuza P Funk Majani ndiye aliyempa AY jina la Mzee wa Commercial baada ya msanii huyo kubadili aina ya muziki wake, pia Majani ndiye aliyemzowesha AY kuvaa kofia. Awali alikuwa sio mpenzi sana wa kuvaa kofia.


2. Wimbo wa AY, Zigo Remix umetengenezwa na maprodyuza watatu ambao ni Nahreel, Marco Chali na Harmy B, kitu kama hicho pia kimefanyika kwenye wimbo wa Rayanny, Chombo ambao umetengenezwa na S2kizzy, Rash Don na Laizer.

Hata hivyo wimbo wa AY hauna ‘sign tune’ ya prodyuza yeyote kati ya hao watatu wakati ule wa Rayvanny ukiwa na za maprodyuza wote.


3. Kampuni ya Ogopa Video kutoka Kenya imempatia AY tuzo mbili kwa video mbili walizosimamia, mwaka 2007alishinda Kisima Music Awards katika kipengele cha ‘Best Video’ kupitia wimbo wake, Usijaribu. Vilevile mwaka 2012 alishinda Channel O Music Video Awards kama ‘Best East African Video’ kupitia wimbo Don’t Wanna Be Alone. Zote wameongoza Ogopa Video.


4. AY na Diamond walisafiri kutoka Tanzania hadi Afrika Kusini kufanya video ya wimbo Zigo Remix lakini bado ulikuwa haujarekodiwa. Baada ya kuwasili Afrika Kusini ndio wakarekodi Zigo Remix wakiwa na prodyuza Harmy B lakini sio studio, bali katika chumba cha hoteli waliyofikia.


5. AY ndiye msanii wa kwanza Afrika Mashariki na wa tatu Afrika kuhojiwa kwenye kipindi cha Focus On Africa cha BBC. Hiyo ilikuwa Juni 2013 ambapo alieleza kuwa amekuwa akifanya vizuri kwenye muziki kwa kipindi kirefu kutokana ni kuchapakazi sana na anauchukulia muziki kama biashara.


6. AY ndiye msanii pekee Tanzania kushinda tuzo za muziki na vyombo vya habari (TV Media). Hilo amelieleza katika wimbo wake uitwao El Chapo. Utakumbuka AY ni miongoni mwa wamiliki wa kipindi cha Mikasi ambacho kimewahi kushinda tuzo mbili kutoka Tuzo za Watu.


7. Baadhi ya vipande vya video ya wimbo wa AY, I Don’t Wanna Be Alone ambao amewashirikisha Sauti Sol kutoka Kenya vimechukuliwa na simu. Hata hivyo, video hiyo ilikuja kushinda tuzo ya Channel O Music Video Awards 2012 kama video vora toka Afrika Mashariki.


8. AY alifika Dar es Salaam mwaka 1999 kwa lengo la kuanza muziki. Pia alishawishiwa zaidi na rafiki yake, G Zingalize ambaye alikuwa anasoma naye Ifunda Technical School Iringa.

Alianza kuishi kwenye kontena Masaki, kisha akahamia kwa kina G Zingalize na baadaye kwa King Crazy GK ambaye walikuja kufanya wote muziki kwenye kundi la East Coast.


9. Sauti ya kike inayosikika kwenye wimbo El Chapo ikimuelezea AY ni nani hasa kwenye muziki ni ya Jokate Mwegelo ingawa kwenye video hajaonekana wala kutajwa kutokana video kutumia ‘version’ nyingine ya wimbo.



10. AY ndiye msanii wa kwanza Tanzania kufanya kazi na Director Godfather toka Afrika Kusini. Hiyo ni baada ya kuona video kali za kundi la P Square, lakini hazikuonyesha nani kazifanya, ndipo akaanza kufuatilia hadi kumpata.

Pia ndiye aliyemkutanisha Shetta na Godfather ambaye alifanya video ya msanii huyo, Kerewa iliyogharimu Dola 10,000. AY alichukua Dola7,000 toka kwa Shetta na kumlipa Godfather kama malipo ya awali ndipo kazi ikaja kufanyika.