Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majizo awatetea wasanii, wadau wamcharukia

MAJIZO Pict

Muktasari:

  • Jambo hilo limemfanya Mkurugenzi wa EFM na TV E, Francis Ciza 'Majizo', kuvunja ukimya na kujitokeza hadharani kuwaomba mashabiki kusitisha vikwazo vinavyoendelea, akionya kuwa hatua hiyo inaathiri mfumo mzima wa muziki, lakini mashabiki wamemjia juu ya kumwambia 'asiwapangie'.

FANI ya muziki Tanzania ikiwamo Bongo Flava inakumbwa na msukosuko, huku wasanii wakubwa wakikabiliwa na lawama kutoka kwa mashabiki kutokana na ukimya wao na kile kinachoonekana kutokujali wakati wa machafuko yaliyotokea baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.

Jambo hilo limemfanya Mkurugenzi wa EFM na TV E, Francis Ciza 'Majizo', kuvunja ukimya na kujitokeza hadharani kuwaomba mashabiki kusitisha vikwazo vinavyoendelea, akionya kuwa hatua hiyo inaathiri mfumo mzima wa muziki, lakini mashabiki wamemjia juu ya kumwambia 'asiwapangie'.

Vikwazo hivyo vimeongezeka baada ya vurugu za Oktoba 29, ambapo nyota wakubwa kama Diamond Platnumz wamepoteza wafuasi kufuatia wimbi la ukosoaji mtandaoni.

Hata hivyo, jana Majizo amesema madhara tayari yanaonekana, akibainisha kuwa baadhi ya wasanii wamepunguza uzalishaji kutokana na vitisho na hofu ya kukataliwa na mashabiki.

Amesisitiza kuwa tasnia ya muziki inaajiri maelfu ya vijana wa Kitanzania na kujiondoa kwa mashabiki kunawaathiri moja kwa moja.

“Kutokusaidia video moja pekee kunaweza kuathiri mamia ya ajira,” aliwaambia mashabiki.

Amehimiza kuwepo kwa mazungumzo ya wazi kutatua mgawanyiko unaoendelea, akiongeza kuwa hata wasanii huru ambao hawakuhusika na sakata hilo nao wanakumbwa na madhara hayo.

Majizo pia aliwaomba radhi mashabiki waliokwazika na lugha kali iliyotumiwa na baadhi ya wanamuziki.

Mara nyingi, watu mashuhuri nchini wamekuwa wakitumika na chama tawala, CCM kupata uungwaji mkono wa umma wakati wa kampeni za kisiasa, jambo ambalo mara kadhaa limekuwa likikosolewa

“Msamaha ninaoomba ni kwa sababu nafahamu kuna mahali wadogo zangu hawa walipitiliza na sio kwa sababu walifanya kampeni (ile ni haki yao na uamuzi wao). Najua kuna maneno yalikukera, sio katika level ya siasa, bali katika level ya utu naomba msamaha, alinukuliwa Majizo na kuongeza;

“Huu muziki ni wenu. Mkiumiza tasnia, mnaumiza maelfu ya ajira. Kina Shilole hao wanaweza kutufikia sisi siku moja moja ukamtoa, vipi kuhusu wale wafanyakazi wake? Diamond na wengine, Mungu amewajaalia riziki, lakini unawaza kuhusu ajira zinazopotea kwa sababu ya hasira yako kwake?”

“Naomba Radhi, na ikiwapendeza naomba muendelee kuupa nguvu muziki wenu”. Haya ni maneno ya Majizo.


WADAU WAMKATAA

Hata hivyo, muda mchache baada ya kauli hiyo ya Majizo wadau wa muziki wakiwamo baadhi ya wanamuziki wakongwe na mashabiki pamoja na wapenzi wa fani hiyo walimcharukia kila mmoja akiwa na maoni yake tofauti.

Mwimbaji wa miondoko ya Hip Hop Tanzania, Wakazi amemjibu Majizo kwa kumtaka atulie na kama kweli alitaka suluhu angewacheki wasanii wakongwe na kumalizana nao kabla ya kuibuka kuwatetea wasanii waliowaacha Watanzania solemba kwa masilahi yao binafsi na ubinafsi.

Pia mkongwe na hip hop na Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' amesema licha ya Majizo kuwa "mwanae sana tu" na alimsadia kumuinua, lakini hakubaliani na alichokifanya cha kuwatetea wasanii wasiojitambua.

Mashabiki na wapenzi wengine wameendelea kusisitiza kama ambavyo wasanii hao walivyowaacha wanaowasapoti katikati ya majonzi na kuwatolea maneno ya kejeli, nao wameamua kuwaacha wafanye kazi maisha yaendelee, ila wasipangiwe cha kufanya na Majizo ama yeyote kwa vile hata wao hawakuwapangia cha kufanya.