Luiza Mbutu, afiwa na muwewe jioni hii
Muktasari:
- Mume wa Luiza ambaye pia ni mwanamuziki amekumbwa na mauti jioni hii akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua na kwa wiki moja.
MWIMBAJI maarufu wa muziki wa dansi nchini, Luiza Mbutu amepata pigo baada ya jioni hii kufiwa na mumewe, Fariala Mbutu.
Mume wa Luiza ambaye pia ni mwanamuziki amekumbwa na mauti jioni hii akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua na kwa wiki moja.
Akizungumza na Mwanaspoti, Luiza ambaye ni Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga Pepeta amesema, Fariala amefariki dunia jioni hii Hospitali ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Luiza amesema, Fariala alikuwa anasumbuliwa presha, lakini ghafla alipata tatizo la tumbo ambalo ndilo limechukua uhai wa mumewe.
"Alikuwa anasumbuliwa na presha tu, ila akaja kuumwa tumbo ghafla likavimba, tukampeleka hospitali ya Muhimbili akafanyiwa vipimo akakutwa na tatizo la mrija wa kupitisha chakula umevimba ikabidi wamfanyie upasuaji wakapunguza utumbo kisha wakaunganisha tena, sasa akawa anaendelea na matibabu ndio akafariki jioni hii," amesema Luiza.
Fariala enzi ya uhai wake alikuwa mpiga gitaa la besi na mmiliki wa bendi ya The Buffalo ambayo ilikuwa inapiga zaidi kazi za hotelini.
Luiza na Faliala walifunga ndoa mwanzoni mwa miaka ya 2000 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Bryan.
Msiba uko nyumbani kwao Salasala jijini Dar es Salaam