Koffi aliamsha kwa Mkapa

Sunday August 29 2021
koffi pic
By Ramadhan Elias

MSANII Nguli wa Muziki wa dansi  kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DR Congo) Koffi Olomide amepiga shoo ya kibabe leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kunapofanyika Kilele cha Tamasha la Yanga ‘Wiki ya Mwananchi’

Koffi aliingia uwanjani hapa saa 11:00 akiwa katikati ya skauti wasiozidi 30 waliomzingira huku akisindikizana na madansa wake watatu wa kike.

Koffi ayekuwa amevaa suti ya kaptula, kofia, soksi na viatu vyote vya njano alishangiliwa na mashsbiki wote waliopo uwanjani hapa pale alipoingia.

Baada ya hapo alielekea katika jukwaa na kuanza kushusha ngoma moja baada ya nyingine huku akianza na ile ya ‘Ekotite’ ambayo ni maarufu sana nchini hapa.

Burudani nyingine katika shoo ya Koffi ilikuwa ni madansa wake wakike watatu namna walivyokuwa wakisakata rumba sambamba na Koffi kwa staili tofauti tofauti.

Jukwaani pia mashabiki wa Yanga hawakupoa kwani nao waliendelea kumshsngilia huku wengine wakisakata rumba kama kawaida.

Advertisement

Shoo ya Koffi ilidumu kwa dakika 17 kisha alifunga na kuondoka.

Advertisement