Kisa maadili, Wema aitwa Bodi ya Filamu

Muktasari:
- Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk Gervas Kasiga imemtaka msanii huyo kufika katika ofisi za bodi hiyo Mei 22, 2025 saa 4 asubuhi kwa ajili ya mahojiano.
Bodi ya Filamu Tanzania imemuita msanii Wema Sepetu kwa ajili ya mahojiano kuhusu picha jongefu zilizorushwa kwenye mtandao wa kijamii zikionyesha amevaa mavazi yasiyo na staha.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk Gervas Kasiga imemtaka msanii huyo kufika katika ofisi za bodi hiyo Mei 22, 2025 saa 4 asubuhi kwa ajili ya mahojiano.
Bodi ya Filamu Tanzania inaendelea kuwasihi wasanii wa filamu kuendelea kulinda maadili ya nchi katika kazi za tasnia pamoja na mienendo yao kijamii.
Siku tatu zilizopita Wema alionekana akiwa amevaa vazi ambalo linadaiwa kwamba halikuwa na staha kwenye sherehe ya kujipongeza kupata Tuzo ya Thamani nchini Kenya.