Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinachomtesa Mbosso hiki hapa

MBOSSO Pict

Muktasari:

  • Imekuwa kawaida, Mbosso kusimulia kisa cha mpenzi wake huyo ambaye anadai alikuwa akimfumania mara kwa mara lakini aliendelea kuwa naye kutokana na mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo.

NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Mbosso, amefichua kitu kinachomtesa kwa sasa ni mpenzi wake wa zamani ambaye anashindwa kuacha kumzungumzia kila awapo katika mchanganyiko wa watu.

Imekuwa kawaida, Mbosso kusimulia kisa cha mpenzi wake huyo ambaye anadai alikuwa akimfumania mara kwa mara lakini aliendelea kuwa naye kutokana na mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo.

“Naweza kuonekana nimechanganyikiwa na hii najua hamtanielewa kwanini kila wakati napenda kuongelea hili suala la mpenzi wangu wa zamani niliyemfumania halafu nikaendelea kuwa naye, nyie mapenzi yana nguvu sana na yananitesa na wala sio masihara, hapa ndio niliamini kwa watu hawaachani sababu ya udanganyifu, wanaachana sababu mapenzi yamekwisha,” alisema Mbosso.

Mbosso, hivi karibuni alitoa ushuhuda wa maisha yake ya mapenzi alipokuwa akitumbuiza katika tamasha la Yamaha Concert. akiwa jukwaani, Mbosso alizungumzia wimbo wake maarufu Limevuja, akieleza kuwa ni moja ya nyimbo zinazobeba uhalisia wake.

 Katika maelezo yake ya kihisia, Mbosso ndipo alisimulia jinsi alivyowahi kumfumania mpenzi wake mara kwa mara lakini akaendelea kuwa naye kutokana na mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo.

Nyota huyo ni zao la kituo cha Mkubwa na Wanae kilichokuja kuzaa Yamoto Band iliyokuwa ikiundwa na Beka Flavour, Dogo Aslay na Enock Bella.