Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kali za 2025, huko mitandaoni zimekimbiza balaa

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Siyo hivyo tu, ni mwaka ambao umeshuhudiwa wsanii wakitoa albamu na EP zao na katika hizo, zipo nyimbo zilizofanya vizuri na kpata mapokeo makubwa kuanzia YouTube, Apple, Spotify, Shazam na hata katika mitandao ya kijamii kama TikTok zikihesabu namba za kutosha.

MWAKA 2025 unaisha na baadhiya wasani wakijivunia mafanikio walyoyapata, ukifunga pia milango kwa wasani wachanga akiwamo Dogo Paten.

Siyo hivyo tu, ni mwaka ambao umeshuhudiwa wsanii wakitoa albamu na EP zao na katika hizo, zipo nyimbo zilizofanya vizuri na kpata mapokeo makubwa kuanzia YouTube, Apple, Spotify, Shazam na hata katika mitandao ya kijamii kama TikTok zikihesabu namba za kutosha.

Hapa, Mwanaspoti linakuletea nyimbo 10 bora za mwaka huu, jinsi zilivyofanya vizuri kwenye majukwaa mbalimbali kuanzia video na audio.


1. PAWA-Mbosso

Ni moja ya nyimbo zilizovuma zaidi mwaka 2025, ukithibitisha kwa nguvu sauti ya msanii huyu wa Ep ya Room Number 3 na uwezo wake wa kuunda melodi zinazogusa hisia za mashabiki. Nyimbo hii ilikubalika sana kutokana na ulinganifu wake wa kipekee kati ya midundo ya upendo na rhythm za kisasa za Bongo Flava, ikifanya iwe wimbo wa uliopigwa sana kwenye maharusi, sherehe za kifamilia na hata matukio ya redio na TV.

Upekee wa wimbo huo unaonekana pia kwenye mitandao ya kijamii na mashabiki walijumuika katika kushiriki kwa kuimba vipande vya video fupi za wimbo huo, kufanya chalenji au kuunganisha na sherehe zao binafsi.

Wimbo huo hauhitaji maelezo mengi ili kuonyesha ubora huo ulifanya vizuri  YouTube kwa kusikilizwa na kutazamwa sana hadi sasa umevutia takriban milioni 51 za watazamaji, jambo linaloonyesha nguvu ya mvuto wake.

Nyimbo hiyo pia ilishika nafasi ya juu kwenye playlist za Apple Music Tanzania na Spotify, ikionyesha haikuwahi kupitwa na mashabiki wa muziki wa Kiswahili.


2. MVUA -Marioo

Marioo alikuwa mmoja wa wasanii walioongoza mwaka huu na nyimbo ya “MVUA” ilivuma sana kwenye Apple Music Tanzania na YouTube.

Katika mtandao wa Youtube nyimbo hii ilipata watazamaji milioni 5.7, Apple Music ikapata milioni 2.1, wakati Spotify ni milioni 1.3.

Katika mtandao wa TikTok, nyimbo hii pia ilishika kasi na zikatengenezwa video 800,000.


3. ALONE -Rayvanny & Headie One

Ni ngoma iliyovuka mipaka ya Tanzania hadi barani Ulaya. Rayvanny alitia maneno ya kiswahili wakati rapa wa Uingereza Headie One akitia maneno ya Kiingereza.

Katika Apple Music International, nyimbo hii iliingia katika tano bora kwa wiki kadhaa, vilevile Shazam iliingia katika nyimbo 20 bora za Afrika Mashariki, huku Spotify Global ilikuwa na wasikilizaji milioni 3.2.


4. KATAM-Diamond Platnumz ft. Bien

Nyimbo hii ndiyo moja ya ngoma zilizovuma sana mwaka 2025, ikichanganya midundo ya Bongo Flava na Afrobeat kwa mtiririko mzuri. Ilichaguliwa sana kwenye redio, parties na mikutano mbalimbali, ikichangia kwa kiasi kikubwa kwenye ueneaji wa muziki wa Wasafi.

Katika mtandao wa Youtube imepata takriban watazamji milioni 13.

Apple Music Tanzaniam, nyimbo hii ilifanya vizuri na kufika nafasi tatu za juu katika Charts za Bongo Flava, pia Spotify ilikuwa na wasikilizaji milioni 1.8M huku TikTok zikiwa zimetengezwa jumla ya video milioni 2.5 wakifanya chalenji yake.


5. LALA-Harmonize ft. Abigail Chams

Utengenezaji wa mistari yenye urafiki mzuri wa wawili hao umefanya wimbo huu kuwa hit kwa radio, TV na mitandao huku ukijengea nafasi ya kipekee kwa mashabiki.

Ushirikiano kati ya Harmonize na Abigail Chams umeunda mchanganyiko wa midundo ya kisasa na melodi tamu, ukilenga hisia za upendo, starehe na burudani kwa mashabiki wa muziki wa Kiswahili. Mistari yao inaufanya wimbo huu kuwa rahisi kusikiliza, kuimba pamoja na hata kucheza kwenye pati na sherehe mbalimbali.

Wimbo umevutia takriban watazamaji milioni 30, ikithibitisha mvuto wake mkubwa kwenye mtandao wa YouTube, Spotify wanakadiriwa kufikia wasikilizaji milioni 5.8, jambo linaloonyesha umaarufu wake kimataifa pia.

Wakati kwa upande wa Apple Music Tanzania wimbo umefikisha wasikilizaji milioni 3, ukiweka nafasi ya juu kwenye playlist za Bongo Flava, TikTok zaidi ya video 900,000 zimetengenezwa zikitumia wimbo huu, ikionyesha jinsi mashabiki walivyoshirikiana na trend za kijamii.


6. AMANDA-Zuchu

Ni nyimbo nyingine ya Bongo Fleva ambayo ilitikisa sana ndani na nje ya Tanzania. Nyimbo hii iliyoimbwa na msanii Zuchu, licha ya kwamba hadi sasa haijatolewa video rasmi, imeendelea kukimbiza katika mitandao mbalimbali ya kijamii na majukwaa ya uuzaji wa muziki.

Kule YouTube ingawa haijatolewa video yake rasmi, katika Audio iliyowekwa Youtube hadi sasa ina watazamaji milioni 13.

Kupitia Spotify ngoma hii imesikilizwa mara milioni tano, Apple Music mara milioni 4.7 na kukawa na video fupi fupi laki saba zilizotengenezwa na mashabiki katika mtandao wa TikTok.


7. SALAMA- Barnaba ft. Diamond Platnumz

Ni colabo ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva mara baada ya wawili hao kuachia wimbo huo ambao ulileta mchanganyiko wa ubunifu wa Barnaba na nguvu ya Diamond, inayovutia kwa nguvu ya mashairi na muundo wa Swahili pop.

Tangu wimbo huo umeachiwa una miezi mitatu sasa kutokana na mapokeo yake Youtube na hadi gazeti hili linapelekwa mtamboni ilikuwa na jumla ya watazamaji milioni 26, Spotify milioni 5, Apple Music milioni 4.7 na TikTok umevanyiwa chalenji kwa video zaidi ya laki saba.


8. NO STRESS -Nandy

Wimbo huu unalenga kuhamasisha mashabiki kupunguza mawazo, kukabiliana na changamoto za kila siku kwa mtazamo chanya.

Mistari yake rahisi na melody ya kuvutia inafanya wimbo huu kuwa rahisi kuimba pamoja, kucheza na kushiriki kwa urahisi mtandaoni. Nandy aliendelea kushika nafasi yake kama msanii wa kike mwenye nguvu mwaka huu kwa wimbo huo.

Ilikuthibitisha ukubwa na mapokeo mazuri kutoka kwa mashabiki wimbo huo una watazamaji milioni 3. Spotify 1.2 milioni, Apple Music Tanzania zaidi ya laki tisa na TikTok imetengenezewa chalenji zaidi ya video 300.


9. DUNIA-Marioo

Wimbo huo ulibeba ujumbe wa maisha, changamoto na mashairi yenye kina, jambo lililovutia wengi, hasa vijana wanaotafuta nyimbo zinazowaamsha kisaikolojia na hisia. Mtiririko wa melody ya wimbo huu na beats zake rahisi lakini zenye mvuto umefanya DUNIA kuwa wimbo unaoendana na maisha ya kila siku, sherehe, na hafla za kijamii.

Kwa mujibu wa tathmini ya muziki wa 2025, 'DUNIA' ni mojawapo ya ngoma ambazo zinatajwa kuwa wimbo bora kutokana na ujumbe wake wa maisha na mashairi yenye kinzani.

Kuthibitisha ubora wa mashairi hayo na kuwa kivutio cha wasikilizaji na watazamaji wimbo huyo wa Dunia una wafuasi milioni tisa Youtube, Spotify: 3.5 milioni, Apple Music Tanzania 2.8 milioni na TikTok video  zaidi ya laki nne zilizotengenezwa na mashabiki zikihusisha wimbo huo.


10. TETE-Marioo

Wimbo huo umeendelea kuthibitisha ubora wa msanii huyo kutoa nyimbo nzuri za kuteka hisia za mashabiki. Video yake rasmi ilionyesha pia ubunifu wa kisanaa, ikiwemo Marioo akiwa na mzazi mwenzake Paula Kajala, jambo lililoongeza mvuto wa wimbo huu mtandaoni.

Melodi ya wimbo ni ya kuvutia, rahisi kuimba pamoja na biti zake zinavutia mashabiki wa rika zote, kuanzia vijana hadi watu wazima. Marioo aliongeza wimbo mwingine kwenye orodha ya ngoma zilizofanikiwa mwaka huu na kuonyesha ustadi wake katika kuifanya Bongo Flava ikue na kubadilika.

Wimboi huu ambao katika video amecheza na mzazi mwenzake Paula Kajala hadi sasa ina wafuasi milioni 35. Spotify 8 milioni, Apple Music 6.5 milioni huku kwa upande wa TikTok zimetengenezwa video milioni moja zikionyesha wakifurahia wimbo huo kwa kuuimba.