Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kajala, Vera Sidika watamnyima sana usingizi Konde Boy

New Content Item (1)
New Content Item (1)

STAA wa Konde Music Worldwide, Harmonize ameachia video ya wimbo wake 'Single Again' chini ya Director Kenny, chupa hilo ni uthibitisho kuwa Kajala Masanja na Vera Sidika kutoka nchini Kenya watazidi kumnyima usingizi Konde Boy.

Single Again ni wimbo wa kwanza kutoa Harmonize tangu kuachana na mchumba wake, Kajala aliyemvisha pete Julai 2022 ikiwa ni muda mfupi baada ya kurudiana, kuachana na Kajala ndiko hasa kamechochea kuandika ngoma hiyo.

Katika video ya wimbo huo ameonekana mrembo wa Bongo Movie 'Caren Simba' ambaye anafananishwa na Kajala hasa upande wa shepu yake, kwa mujibu wa Harmonize, Director Kenny ndiye alitoa wazo la kumtumia Caren ambaye ameitendea haki nafasi hiyo.

Hata hivyo, kama Kenny asingetoa wazo hilo, Caren ni aina ya warembo anaowapenda Harmonize na amekuwa akieleza hilo kwenye nyimbo zake kwa miaka mingi, hivyo kumtumia ni ushahidi bado Harmonize anatii kiu ya nafsi yake iliyompeleka kwa Kajala.

Katika wimbo 'Woman' ambao Harmonize kashirikishwa na Otile Brown kutokea nchini Kenya, anaeleza jinsi anavyopenda wanawake wenye shepu mfano wa Caren, Kajala na Vera, hao ndio wamekuwa wakimnyima usingizi na wataendelea kufanya hivyo.

"Nishawahi kujaribu kupapasa, Dar es Salaam, Nairobi hadi Mombasa, sijamuona hadi sasa, wa kufanana na huo mshepu sasa" anaimba Harmonize katika wimbo huo uliotoka kipindi yupo na Kajala.

Ikumbukwe Kajala ndiye mwanamke ambaye Harmonize kumwimbia sana kwenye nyimbo zake ambazo ni sita; Ushamba, Vibaya, Mtaje, You, Deka na Nitaubeba ambayo katika video yake Kajala katokea.
Kabla mapenzi yake na Kajala hayajaanza kuonekana hadharani hapo Februari 2021, Kajala alikuwa akilini kwa Harmonize tangu Agosti 2017 na kupitia wimbo wa WCB Wasafi, Zilipendwa, Harmonize alimtaja Kajala kwa mara ya kwanza.

Wakati huo alikuwa na mpenzi wake, Sarah ambaye walikuja kufunga ndoa mwaka 2019 na baada ya kuachana ndipo akawa na Kajala, na hata walipoachana akawa na Briana, bado nafsi yake haikutulia huko kwani alirudi tena kwa Kajala na kumvisha pete ya uchumba.

"Tena ni mtu wa Gym, shepu ndio linanipa wazimu," anaimba Harmonize katika wimbo wake uliomwimbia Kajala 'Mtaje' unaopatikana kwenye albamu yake ya pili, High School (2021).

Katika wimbo wake, Show Me uliotoka Aprili 2017 akimshirikisha Rich Mavoko, Harmonize aligusia jinsi anavutiwa na warembo aina ya Vera Sidika kutokea nchini Kenya, utakumbuka Vera anasifika kuwa na umbo nzuri linalovutia wanaume wengi.

"Wakati unakwenda au unarudi wakata kona, nyuma ka katuni za masudi ulivyonona.... Anita macho kama unaniita, saa sita shepu Vera Sidika," anaimba Harmonize katika verse ya kwanza tu ya wimbo huo.
Utakumbuka Vera alianza kuvuma Afrika Mashariki mara baada ya kutokea kwenye video ya wimbo wa kundi la P Unit 'You Guy' iliyotoka takribani miaka 10 iliyopita ila shepu yake ndiyo hasa imemfanya kuwa maarufu na kumnyima usingizi Konde Boy.

Hivyo Director Kenny kuja na wazo la kumtumia Caren katika video hiyo ni kama tayari alishaisoma akili ya Harmonize na kujua kipi anakitaka katika maisha yake na muziki wake.
Na kweli Caren kafanya vizuri katika video hiyo kwa kucheza kama Ex wa Harmonize ambaye ni Kajala, tazama namna alivyovaa na kutengeneza nywele zake.

Ikumbukwe wimbo 'Single Again' umekuwa ukifanya vizuri sana TikTok ambapo amevuma (trend) kwenye nchi zaidi ya 15 duniani na ni wimbo wa kwanza wa Harmonize kupata mapokezi hayo miezi ya hivi karibuni. Nchi hizo ni kama Nigeria, Morocco, Canada, Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Uhalonzi, Denmark, Sauti Arabia n.k.