Jay Moe, Ferouz watua Mbeya City

Muktasari:
- Shangwe hilo la Mbeya City linafanyika kesho kwenye Ukumbi wa City Pub Kiotani jijini Mbeya ili kutoa pongezi kwa kikosi cha timu hiyo kilichorejea Ligi Kuu, baada ya kushuka msimu wa 2022-2023.
WAKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Jay Moe, Ferouz na Dullayo ni miongoni mwa wasanii waliotua jijini Mbeya ili kunogesha pati ya Mbeya City iliyopanda Ligi Kuu kwa msimu ujao.
Shangwe hilo la Mbeya City linafanyika kesho kwenye Ukumbi wa City Pub Kiotani jijini Mbeya ili kutoa pongezi kwa kikosi cha timu hiyo kilichorejea Ligi Kuu, baada ya kushuka msimu wa 2022-2023.
Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Mbeya City, Gwamaka Mwankota alisema wasanii mbalimbali watainogesha pati hilo akiwamo Mchizi Mox, Afande Sele, Soggy Doggy na MB Dog.
“Tutakuwa na mambo mengi ila kubwa zaidi ni wasanii kutoa burudani kwa wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wetu kwa kufanikisha adhima yetu ya kurejea Ligi Kuu, niwaombea wadau wa Mbeya na mikoa ya karibu kujitokeza kwa wingi,” alisema Mwankota.
“Tumeweka kiingilio rafiki kiasi cha Sh 10,000 tukiamini kila mmoja wetu ataweza kukimudu na kuhudhuria tukio hilo kubwa na la kihistoria, tumeweka burudani ili kuthamini mchango mkubwa uliofanywa na wachezaji wetu na benchi letu la ufundi.”
Mbeya City imepanda Ligi Kuu kutok Ligi y Championship sambamba na Mtibwa Sugar iliyokuwa imeshuka msimu uliopita ikiwa na Geita Gold.