Jay Melody ampora Shilole Sh30 milioni studio

Monday June 13 2022
jay pic
By Peter Akaro

MKONO wake upande wa uandishi umeweza kutengeneza ngoma kubwa ndani ya Bongofleva. Sauti yake imeibua shangwe na msisimko wa aina yake katika masikio ya mashabiki wa muziki huo.

Ni Jay Melody ambaye ana miaka mitano tangu atoke kimuziki, lakini miaka miwili ya mwisho imekuwa yenye mafanikio makubwa zaidi kwake baada ya kuachia ngoma zake tatu Huba Hulu, Najiweka na Sugar. Bongo Music Facts inakujuza zaidi:


1. Jina la Jay Melody alipewa na Ruge Mutahaba alipojiunga Tanzania House of Talent (THT) ambapo ndipo alitoa wimbo wake kwanza, Goroka uliomtoa kimuziki.


2. Ukiachana na muziki, vipaji vingine vya Jay Melody ni uchoraji na uchezaji soka sawa na Alikiba aliyecheza Coastal Union na Ruby aliyekipiga Young Twiga Stars.

Advertisement


3. Licha ya wimbo wa Jay Melody, Huba Hulu kuchukua kidogo vionjo toka kwenye ngoma ya Amr Diab iitwayo El Habayib, kukuwasiliana naye kumjulisha hilo.


4. Miongoni mwa ndoto kubwa za Jay Melody ni kununua gari ya Rolls Royce ambalo hapa Bongo msanii aliyelimiliki ni Diamond Platnumz tu, Afrika kuna kuna Davido, Burna Boy na wengineo.


5. Kwa kipindi cha miezi mitatu tangu ulipotoka wimbo wake, Sugar uliweza kuingizia Sh30 milioni ukiwa ndio wimbo wake wa kwanza kufanya vizuri kimauzo kwa muda mfupi.


6. Video ya wimbo wa Jay Melody, Wenge iliyotoka Novemba 23, 2019 imefanyika sehemu ambayo ilifanyika video ya Rose Ree, Dow iliyotoka Novemba 10, 2017, hiyo ni kwa scene za mwanzo kwa video zote mbili.


7. Wasanii wa kimataifa ambao Jay Melody anatamani kufanya nao kazi ni Simi, Fireboy na Wiz Kid, hawa wote wanatokea nchini Nigeria.


8. Jay Melody ndiye ameandika verse ya Nandy katika wimbo wa mwimbaji huyo, Do Me aliyoshirikiana na mchumba wake, Bilnass, pia alimwandikia ngoma yake, Kivuruge.


9. Wakati akiwa na njaa ndio Jay Melody anakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuandika nyimbo zake na wasanii wengine, kumbuka ameshawahi kuwaandikia kina Nandy, Benson, Jolie na Nadia Mukami toka Kenya.


10. Wimbo wa Jay Melody, Najiweka ulikuwa wa Shilole aliopanga kumshirikisha msanii huyo, lakini baadaye Jay akaamua kuupora toka Shishi na kuufanya kuwa wake na ndio huo uliokuja kumuingizia Sh30 milioni kwa miezi mitatu.

Advertisement