Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyo Msaga Sumu apewe maua yake

Muktasari:

  • Man Fongo amesema wapo baadhi ya wanamuziki wa Singeli akiwemo yeye, hupenda kujiita wafalme wa singeli kila mara, hasa wanapowika kwa kazi moja ama mbili, lakini ukweli, wanamkosea heshima Msaga Sumu kwani ndiye anayestahili cheo hicho hata kama wengine hawapendi.

NYOTA wa muziki wa singeli nchini, Man Fongo amesema bila kuuma maneno au kupepesa macho, mkongwe wa miondoko hiyo, Msaga Sumu anastahili apewe heshima ya ufalme wa muziki huo kutokana na makubwa aliyofanya kabla ya kuibuka wasanii wengine.

Man Fongo amesema wapo baadhi ya wanamuziki wa Singeli akiwemo yeye, hupenda kujiita wafalme wa singeli kila mara, hasa wanapowika kwa kazi moja ama mbili, lakini ukweli, wanamkosea heshima Msaga Sumu kwani ndiye anayestahili cheo hicho hata kama wengine hawapendi.

"Naweza sema ni vibe au sifa za mashabiki zikizidi kwa baadhi yetu sisi wanamuziki wa Singeli kujipa taji la ufalame ikiwa heshima hiyo anatakiwa kupewa Msaga Sumu kutokana na makubwa aliyofanya kwenye muziki huo kabla ya kuibuka wasanii wengine," alisema staa huyo wa Hainaga Ushemeji, Kibaka na Umesikia.

Msaga Sumu ambaye majina yake kamili ni Seleman Jabir aliyeanza muziki zaidi ya miaka 10 iliyopita baada ya kuachana na biashara ya mitumba aliyokuwa akiifanya, anatamba na ngoma kadhaa zikiwamo Tabia Mbaya, Cheupe Dawa, Unanitega Shemeji, Mwanaume Mashine na Dodoki bado anaendelea kusumbua licha ya kuwepo vichwa mbalimbali katika miondoko hiyo iliyiojizolea umaarufu ndani na nje ya nchi.