Hamisa Mobetto, Rick Ross penzini?

Friday November 26 2021
Hamisa PIC
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Mwanamitindo Hamisa Mobetto na msanii toka Marekani Rick Ross mapenzini? Hivi ndivyo unavyoweza kujiuliza baada ya wawili hao kuonekana wakiwa pamoja.

Picha za wawili hao zilianza kusambaa mitandaoni usiku wa jana Jumatano Novemba 25, 2021 wakiwa katika falme za kiarabu Dubai wakila bata pamoja.

Moja ya picha zilianza kuwashtua watu ni jana mchana ambapo picha zilizotumwa za wawili hao zote zilionekana zikisoma Dubai.

Usiku pia wawili hawa walionekana wakicheza muziki kwenye moja ya kumbi za starehe kwa kukumbatiana kimahaba.

Kama haitoshi wakati wa kuondoka kwenye ukumbi huo, Hamisa alionekana akipita kuelekea kupanda kwenye gari iliyokuja kumchukukua Rick Ross aina Rolls Royce.

Advertisement

Hata hivyo video zingine zikamuonyesha Hamisa akiwa ndani ya gari wakiendeleza mahaba na msanii huyo aliyewahi kutikisa na ngoma mbalimbali ikiwemo Hustlin, B.M.F., Maybach, Tears of Joy, I'm Not A Star na nyingine nyingi.

Swali bado linabaki ni kweli wawili hawa wapo penzini au wapo kikazi maana na dada yetu Hamisa sikuizi anaimbaa?


Endelea kufuatilia Mwanaspoti kupata habari zaidi.

Advertisement